Wakatoliki mnakwama wapi kwenye media?

hHAHAAAAAAA, Yesu alisema, Yohana mbatizaji alibatiza kwa maji, ila ubatizo wake yeye ni wa Roho Mtakatifu. lakini ninyi mnabatiza kwa mshumaa na kitambaa cheupe
Ni muendelezo wa niliyosema mwanzo, theolojia na falsafa, au kwa ufupi ELIMU. Wewe hapo umeona mshumaa, werevu wanaona mwanga! Wewe umeona kitambaa cheupe, werevu wameona usafi wa moyo!
 
Ni muendelezo wa niliyosema mwanzo, theolojia na falsafa, au kwa ufupi ELIMU. Wewe hapo umeona mshumaa, werevu wanaona mwanga! Wewe umeona kitambaa cheupe, werevu wameona usafi wa moyo!
hapo hapahitaji mwerevu, Neno la Mungu lipo wazi, unajazwa Roho Mtakatifu na unanena kwa lugha, sasa hebu tueleze, huo mshumaa mkiufanyiza hivyo mnavyoufanya huwa mnanena kwa lugha? what is the manifestation kwamba mtu sasa amejazwa Roho Mtakatifu kama Yesu alivyoagiza, ishara gani mnaziona. Jibu hilo swali.
 
unaongea lugha ambayo wewe hauielewi kwasababu roho yako ndio inakuwa inaomba, mwili hauna faida hapo, unaongea mambo yako ya binafsi ya rohoni, ndivyo ilivyoandikwa. ila kama hauongei kwa manufaa binafsi, unatakiwa kutafsiri ili wale wanaotakiwa pia kunufaika wasikie. sasa kama naomba mambo yangu binafsi, wengine wasikie ya nini?

1Korintho 14: 14 Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda. 15 Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia. Maana ni kweli, wewe washukuru vema, bali yule mwingine hajengwi. 18 Namshukuru Mungu ya kuwa nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote; 19 lakini katika kanisa napenda kunena maneno matano kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, kuliko kunena maneno elfu kumi kwa lugha.

sasa, ninyi hata hayo matano mliwahi kujazwa mkanena? ulishawahi kuona padre amenena? why? jibu swali hili.
 
Ni jibu tosha hilo
Mungu akupe uelewa uone tunachoongea ni cha maana sana kwenye maisha yako. hakuna anayetangaza dini, sina kanisa, mimi sio mchungaji na dini yangu pia niliyonayo siwezi kusema ipo perfect, ila kwasababu nimefunzwa kusoma Neno na Mungu ananisaidia kulitafsiri, icho ndio nashukuru Mungu, ninachotangaza hapa ni ukweli wa Neno la Mungu. huwezi kuishi hapa duniani ukashinda dhambi bila kuwa na Roho Mtakatifu, na huwezi kusema una Roho wakati hajawahi hata kujidhihirisha kama Yesu livyosema. Yesu alisema mtanena kwa lugha. Paulo anaeleza kwamba kunena kwa lugha ni muhimu kwani roho yako inakuwa inaomba, kama huna hautaomba mambo ya rohoni bali ya mwilini ambayo majority huwa ni tamaa za dunia na si mapenzi ya Mungu na hivyo maombi yako hayatajibiwa. Mitume walijazwa Roho wakanena, kote walikohubiri watu walijazwa Roho na kunena, kwanini leo hakuna udhihirisho kwenye kanisa katoliki la kunena? tuseme ndio lile lile la kina Petro walio nena, Paulo walio nena n.k? vinafanana kweli? mbona kama havifanani? kimbiaaaaa, hapo mmekalia dini iliyoshikilia mapokeo ya wanadamu yasiyookoa.
 
Kwa nini unakomalia kunena kwa lugha kama ndio ishara ya kujazwa Roho Mtakatifu? Kwani yale maneno hayawezi kutamkwa na msanii yeyote? Mbona ni yale yale bobosha braka patratrata?
 
unaongea lugha ambayo wewe hauielewi kwasababu roho yako ndio inakuwa inaomba, mwili hauna faida hapo, unaongea mambo yako ya binafsi ya rohoni, ndivyo ilivyoandikwa.
Kama unaongea kwa manufaa yako, basi usiwasingizie Mitume, maana wao waliongea kwa manufaa ya watu wengine. Kwa ufupi mnachofanya ninyi lengo lake ni tofauti na walilofanya mitume. Wao mitume Roho wa Bwana aliwapa ujasiri wa kutangaza neno la Mungu kwa mataifa mbalimbali (kama walivyofanya Wamisionari), wakatoka nje maana walikuwa wamejifungia, wakawahubiria watu bila uoga habari za Kristu. Wewe unasema Roho wa Bwana anawafanya muongee mambo yenu ya binafsi! Ajabu
 
Wazo zuri lifanyiwe kazi.
 
ndugu yangu, sijui wewe ni padre au ni muumini au nini, kama ni muumini, nahisi unatakiwa sana kusoma Neno la Mungu, na kama ni padre kwasababu huwa mnasoma miaka mingi, nasikitika kusema kwamba miaka yote hiyo ulipoteza bure.

hayo maneno sio mimi niliongea, ni Mtume Paulo kwenye nyaraka zake, nimekuja nikukuwekea mistari hadi inachosha sasa. Mitume ndio walifanya hivyo. Petro kwani hakuwa mtume? kwenye huduma yake alifanya hivyo, Paulo naye kwa utume wake wa aina yake ila alikuwa mtume, je? hakufanya hivyo?
 
Kwa nini unakomalia kunena kwa lugha kama ndio ishara ya kujazwa Roho Mtakatifu? Kwani yale maneno hayawezi kutamkwa na msanii yeyote? Mbona ni yale yale bobosha braka patratrata?
Kwasababu Neno la Mungu ndivyo linavyosema, hiyo ni mojawapo ya ishara.
MARKO 16:17 inasema, Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa Jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya".

hivi wewe huu mstari unaufahamu? ulishawahi kuuona? unafikiri unamaanisha nini? au ni kwasababu tu hamumpendi Roho Mtakatifu? au unashaurije, huu mstari tusiwe tunauamini au kuufuata ulivyo? tuutoe kwenye Biblia, au tufanyeje, sema.
 
Kwa hiyo bubu hawezi kujazwa Roho Mtakatifu?
 
Kwa hiyo bubu hawezi kujazwa Roho Mtakatifu?
anajazwa, kwanini asijazwe? shida ni kwamba dini yako imekuelekeza kwamba kunena ni mapepo wakati mstari huo hapo wanauona, wangelikuwa walishawahi kunena walau hata mara moja wangelijua kuwa kunena kwa lugha sio lazima utamke matamshi yoote, ni vile Roho mwenyewe atakavyopenda, hata ukiunguruma tu yeye amependa, hivyo hata Bubu anaweza kunena kwa jinsi ile yeye alivyo na vile Roho apendavyo. hata wasio mabubu huwa wanaena kwa matamshi na mengine yasiyo matamshi pure.

hilo swali ulitakiwa uulizwe wewe unayesema lugha lazima wengine wasikie, sasa bubu kiziwi atasikiaje?, kutafsiri ni kweli ila sio kwa maeneo yote, ukiwa unasali peke yako utaamua uombe kwa akili na uombe kwa lugha pia kwasababu unasali juu ya nafsi yako kibinafsi, ila ukiwa unaomba kwa kuhudumia wengine hapo tafsiri ndio inahitajika, ndivyo Neno la Mungu lilichomaanisha. hata hivyo, nimekuwekea mistari, nitakuwekea tena, pengine kuna siku utaelewa.

MARKO 16:17 inasema, Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa Jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya".
 
Acha uongo sidhan kama kuna Radio kwa sasa yenye Masafa mengi kwa sasa kama radio Maria.
Jamaa haongelei masafa kuwa mengi, je huko inakofika watu wanaisikiliza..?

Radio Maria vs clouds
Radio Maria vs efm
Radio Maria vs wasafi
Radio Maria vs radio sauti ya injili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…