Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Wakazi wa familia zaidi ya 700 wa Udindivu, Mtaa wa Kizimkazi, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani, wamefungua kesi ya madai katika Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo wakidai kubomolewa nyumba zao bila kufuata taratibu za kisheria.
Wananchi hao wanasema hatua hiyo imewaacha bila makazi, huku baadhi wakilazimika kuishi chini ya miti ya mibuyu. Wamedai ubomoaji huo ulifanywa kwa kisingizio cha kuwafukuza ili kupisha shughuli za uchimbaji wa mchanga.
Mmoja wa waathirika, Gabriel John, amesema walivunjiwa nyumba na kuharibiwa mali zao kwa madai kuwa wanawaweka wachimbaji wa mchanga, jambo ambalo anadai ni mpango wa kuwafukuza ili biashara hiyo ifanyike katika maeneo yao.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga akizungumza na Jambo TV kwa njia ya simu ameeleza kuwa anafahamu kuhusu shughuli za uchimbaji wa mchanga huku akifahamu kuwepo kwa mgogoro wa ardhi katika eneo hilo akisema hawezi kulizungumzia zaidi kutokana na kuwepo kwa kesi mahakamani katika eneo hilo.
Wananchi hao wameiomba Serikali kuingilia kati mgogoro huo na kuhakikisha wanatendewa haki, wakisisitiza kuwa hali waliyo nayo sasa ni mateso makubwa kwa familia zao.