Kumsaidia bwana mdogo Wakazi ni kuwa, Ngwea sio Rapa tu bali ni full package.
Kwa nini? Ngwea ni kifurushi kilicho kamili yaani ukimshinda huku yeye atakushinda kule na pale.
Ngwea ana Rap, ana flow kali, ni mwandishi mzuri, anaimba, anafanya Freestyle kwa kiwango kikubwa nk na pia ni miongoni mwa Rappers wachache wenye hit song nyingi.
Mfano Chid akimzidi Ngwea kwa flow atazidiwa kwa freestyle, Mbishi akimzidi Ngwea kwa freestyle atazidiwa kwa flow, F.A akimzidi Ngwea kwa uandishi basi atazidiwa kwa kuimba nk.
Yaani Ngwea ni package iliyokamilika hivyo ni mtu asiyefananishwa, mfano Prof. Jay, Jay Moe na wengineo ni wakali kwenye Hip hop hasa upande wa story nk lakini hawawezi freestyle.
Fid q, Mwana F.a ni waandishi wazuri lakini hawawezi freestyle.
Nikki Mbishi ni mkali wa uandishi na freestyle lakini bado kuna mengi kwa Ngwea ambayo yeye ama hayawezi au hajayafanya.
Sent from my SM-G532F using
JamiiForums mobile app