Wakazi: Diamond Platnumz ni maarufu ila hajui kuimba, "ukweli unauma mpaka mnanipigia simu za vitisho"

Alikuaje maarufu? Tuanzie hapo labda.

Na kama hajui kuimba, hajui kuimba mziki wa aina gani? Bongo fleva? Kulinganishwa na nani?

Basi ngoja nitafute ela tu
 
Ben Paul, Rama D wanaimba kuklo Diamond
 
Diamond ameshatengeneza fans base yake na kubwa ko Mara nyingi wanao support ni wale shabiki zake


Wewe tafuta msanii wako mshabikie,acha makasiriko
 
Ukiwa critical thinker kwenye jamii ya watu wenye upeo mdogo kama kitenes unakua unaonekana wewe ndio mwehu
Wakaz yuko sahihi kabisa ila watu wamepofushwa na mahaba
Long,short story saw diamond hajui kuimba.

Leta msanii unaemkubali anajua kuimba bongo na EA mwnye tuzo,hit,fan base, streams na kufanya show majukwaa makubwa Zaid ya mondi...

Ukiweza hapo kweli mondi hajui kuimba.
 
Huu mwandiko unaumiza macho mkuu!
 
Hii Tz watu wake wa hovyo sana kuna kitu kinaitwa criticism & constructive criticism ila sasa mtanzania ukimwambia chochote kati ya hicho anakwambia "chuki" unabaki unashangaa wtf chuki ipi tena
 
Ubishi uishe, diamond hauji kuimba.

Anza kuimba we unaejua
 
Huna akili
 
Long,short story saw diamond hajui kuimba.

Leta msanii unaemkubali anajua kuimba bongo na EA mwnye tuzo,hit,fan base, streams na kufanya show majukwaa makubwa Zaid ya mondi...

Ukiweza hapo kweli mondi hajui kuimba.
Mr Nice na diamond wako sawa mkuu usiwe na hype
 
Wakazi ni miongoni mwa wasanii wasio na vipaji kabisa kuwahi kutokea katika nchii hii ila kutokana na exposure aliyo nayo kuanzia kwenye familia hivyo amejikuta anasikilizwa akiongea jambo. Diamond kafanya jambo ambalo limewashinda wasanii wengi duniani. Jambo lenyewe ni kufanya biashara ya muziki. Diamond kachanganya ujasiriamali na kipaji chake ndo leo hii tunamuona ni msanii milionea ambaye automatically wasanii wengi walio nyuma kimaendeleo lazima watamletea zengwe.

P Diddy, Snoop dogg, Dr Dre na Master P hawajawahi kuwa wasanii walioshika namba moja ila tunavyoongea ni miongoni mwa wasanii matajiri zaidi duniani baada ya kujiongeza kwenye biashara ya muziki na nyinginezo. Hata hapo Congo kuna wasanii wanajua kuimba kuliko Koffi Olomide ila kutokana na akili nyingi za kibiashara yule mzee hadi leo anakimbiza kuliko hao wenye vipaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…