Wakazi Jaws Corner: Muungano wa Tanganyika na Zanzibar una manufaa mapana

Wakazi Jaws Corner: Muungano wa Tanganyika na Zanzibar una manufaa mapana

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
Wakazi wa eneo la Jaws Corner, Mji Mkongwe Zanzibar, wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa ziara yake katika eneo hilo, wakisema imewapa faraja na kuthibitisha kuwa ni kiongozi anayewathamini na kuwajali wananchi wa Zanzibar.

Wakazi hao wameeleza kuwa kitendo cha Rais Samia kukumbuka na kutembelea ndugu zake visiwani humo ni ishara ya upendo wa dhati kwa wananchi wa Zanzibar.

Wamefurahishwa zaidi na hatua ya Rais Samia kushiriki mchezo wa jadi wa Bao, wakisema ni ishara ya kuthamini na kuenzi mila na desturi za Wazanzibari. Kwa mujibu wa wakazi hao, kitendo hicho kinaonesha kuwa Rais ni sehemu ya jamii na anaunga mkono uhifadhi wa utamaduni wa asili wa Zanzibar.

Aidha, wakazi wametoa wito kwa vijana wa Tanzania Bara na Zanzibar kuendelea kushirikiana kwa karibu katika kuleta maendeleo na kutumia fursa zilizopo kwa manufaa ya pande zote mbili za Muungano.

Aidha, Wafanyabiashara wa eneo la Jaws Corner nao wamempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya kuliongoza Taifa, hasa katika kuimarisha na kuendeleza sekta ya utalii nchini.

Wamesema jitihada za Serikali katika sekta hiyo zimechangia kuongezeka kwa idadi ya watalii wanaotembelea Zanzibar, jambo lililopanua fursa za kibiashara kwa wauzaji wa bidhaa za utalii katika eneo hilo.

Wamemuomba Rais Samia kuendelea kuimarisha sekta ya utalii, wakisisitiza kuwa sekta hii ina manufaa makubwa kwa wananchi wa Zanzibar — ikiwemo ajira, fursa za biashara na ongezeko la kipato kwa jamii.
 
Back
Top Bottom