Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Hali hizo ambazo zinaendelea baada jeshi la Israel kuingia Gaza na baada ya kurejelewa kwa vita zimewafanya wakazi hao kusema wanaamini Hamas hawawezi kushindwa kwa njia ya vita na wakaitaka serikali ya Benjamin Netanyahu itiliane saini na wapiganaji wa Hamas ili amani ipatikane na wao warudi majumbani mwao.
Kwa sasa wakazi wa miji hiyo wanaokaribia laki moja wamesambazwa kwenye mahoteli zaidi ya 100 kwenye miji mbali mbali ya nchi hiyo maeneo ya katikati.
Wakazi hao wamesema wanatamani warudi makwao ili watoto wao walale vizuri na kuogolea kwenye mabwawa ya nyumba hizo lakini kwa sasa hawawezi kurudi hata wakipewa fursa ya kufanya hivyo kwa hofu ya kudondokewa na maroketi au mabaki yaliyoripuliwa angani.