Uchaguzi 2020 Wakazi wa Dar es Salaam kweli na nyie mtamnyima Magufuli kura?

zagarinojo

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2020
Posts
2,622
Reaction score
2,846
Wana JF habari. Mi sio mwanasiasa Ila Uchaguzi tunaoshiriki ni wengi japokuwa wengine huwa hawapigi kura Ila maneno wanayo mengi kwenye vijiwe.

Kuelekea tarehe 28.10.2020 siku ya jambo la watu Fulani.
Bado najiuliza Kama wana Dar es Salaam nao watashindwa kumpa kura JPM..

Tunatambua wale jamaa wa Buhaya wao hawana masihara kabisa hapati kitu pale mheshimiwa .

Ila sasa kwa wana Dar es Salaam habari katika television zetu zilipambwa kwa kiasi kikubwa na maendeleo ya mkoa huo.

1. SGR(Railway)
2. Mbezi Stand
3. Ubungo FlyOver
4. Kinyerezi
5. The Port
6. Airport

Na mengine mengi ni heri wana Kaskazini wamnyime Ila sio wana Dar..

Ila ngoja tuone wana DSM wanalichukuliaje hili?
 
Hata Buhaya watampa kura nyingi tu. Pesa za tetemeko zimeboresha shule ya sekondari imekuwa ya kisasa na kuna meli zipo ziwa Victoria zinafanya kazi nzuri.

Watu wa Dar hatuna sababu ya msingi ya kumkataa Magufuli, tuna sababu ya kuwakataa wabunge wanaokwenda bungeni kuvaa vitambaa midomoni na kutoka nje ya ukumbi wakiwa wameshachukua posho ya siku.
 
Wagombea wa CCM huwa wanatuambia Tuache Kutegemea Kuajiriwa Na Serikali, Tujitegemee Na Tujiajiri Wenyewe!! Wakati Wao Wanatuomba Kura Ili Tuwape Ajira Waajiriwe Na wananchi.

TUSAIDIANE MAWAZO HAPA VIJANA WENZANGU, HAWA WATU ZIMO KWELI VICHWANI MWAO ?
 
Dar magufuli amewanyanganya makao makuu ya nchi akawadanganya na flyover. Watumishi wote wa wizara, taasisi,serikali yamehamia dodoma.sasa Dar itafanana na Mombasa .majengo dar yatakosa wateja .sasa mpeni kura. Watu wa kimara waliobomolewa kisa hawakupata kura mwaka 2015.

Bandari kavu imepeleka karibu na chalinze mkome kwenda kudokoa bandarini. Maduka ya kubadilisha fedha yote yalifungwa dar. Katika mji ulioathirika na utaendelea kuadhirika milele ni dar.mpeni kura nyingi na wabunge na madiwani.
 
Hata Buhaya watampa kura nyingi tu. Pesa za tetemeko zimeboresha shule ya sekondari imekuwa ya kisasa na kuna meli zipo ziwa Victoria zinafanya kazi nzuri.
Duh! Je hii nayo ni sera ya CCM? Kwamba kama wananchi wanataka shule zao ziboreshwe wasubiri tetemeko liwakumbe, kama wanataka miundo mbinu iboreshwe wasubiri tetemeko liwakumbe...Hizi ni akili za wapi?
 
Wana JF habari. Mi sio mwanasiasa Ila Uchaguzi tunaoshiriki ni wengi japokuwa wengine huwa hawapigi kura Ila maneno wanayo mengi kwenye vijiwe.

Kuelekea tarehe 28.10.2020 siku ya jambo la watu Fulani.
Bado najiluliza Kama wana Dar es Salaam nao watashindwa kumpa kura JPM..

Tunatambua wale jamaa wa Buhaya wao hawana masihara kabisa hapati kitu pale mheshimiwa .

Ila sasa kwa wana Dar es Salaam habari katika television zetu zilipambwa kwa kiasi kikubwa na maendeleo ya mkoa huo.

1.SGR(Railway)
2.Mbezi Stand
3.Ubungo FlyOver
4.Kinyerezi
5.The Port
6.Airport

Na mengine mengi ni heri wana Kaskazini wamnyime Ila sio wana Dar..

Ila ngoja tuone wana DSM wanalichukuliaje hili?
1602362485621.png

1602362518288.png
 
Lissu hatajenga barabara, shule wala zahanati maana hayo ni maendeleo ya vitu
Atakachokifanya ni kuwafukuza wamachinga barabarani maana hayo ndiyo maendeleo ya watu
 
Wagombea wa ccm huwa wanatuambia Tuache Kutegemea Kuajiriwa Na Serikali, Tujitegemee Na Tujiajiri Wenyewe!! Wakati Wao Wanatuomba Kura Ili Tuwape Ajira Waajiriwe Na wananchi.

TUSAIDIANE MAWAZO HAPA VIJANA WENZANGU, HAWA WATU ZIMO KWELI VICHWANI MWAO ?
Ndio mambo ya serikali ya wanyonge hayo mzee baba.
 
Hata Buhaya watampa kura nyingi tu. Pesa za tetemeko zimeboresha shule ya sekondari imekuwa ya kisasa na kuna meli zipo ziwa Victoria zinafanya kazi nzuri.

Watu wa Dar hatuna sababu ya msingi ya kumkataa Magufuli, tuna sababu ya kuwakataa wabunge wanaokwenda bungeni kuvaa vitambaa midomoni na kutoka nje ya ukumbi wakiwa wameshachukua posho ya siku.
Magufuli hategemei kura za wananchi, kura zake za ushindi zipo Jamana Printers.
 
Hata Buhaya watampa kura nyingi tu. Pesa za tetemeko zimeboresha shule ya sekondari imekuwa ya kisasa na kuna meli zipo ziwa Victoria zinafanya kazi nzuri.

Watu wa Dar hatuna sababu ya msingi ya kumkataa Magufuli, tuna sababu ya kuwakataa wabunge wanaokwenda bungeni kuvaa vitambaa midomoni na kutoka nje ya ukumbi wakiwa wameshachukua posho ya siku.
Mkuu zile pesa ndio lilikuwa lengo lake?
Alafu si vizuri kuwaongelea wakazi wa Dar wote kuwa tutampigia kura jiwe wakati hapa ndio kitovu cha wasomi, waelewa wa mambo yanavyoenda. Kingine ukisema hivyo manaake ni kuwa wanaDar wote tunakubaliana na uminywaji wa uhuru na haki za binadamu, kwamba tulifurahia makonda alivyoingia na askari wa usalama wa taifa pale Clouds Tv wakiwa na silaha za kivita, tunakubaliana na kupotea kwa Ben Saanane na vile viroba vya maiti kwenye fukwe za bahari ya Hindi Dar..
Wanadar hawadanganyiki na uboreshwaji wa miundombinu kwasababu huo ni wajibu wa serikali maana inatumia pesa zetu. Tar 28 ni siku nzito na kila mtu ana jambo lake
 
Back
Top Bottom