Uchaguzi 2020 Wakazi wa Dar es Salaam kweli na nyie mtamnyima Magufuli kura?

Uchaguzi 2020 Wakazi wa Dar es Salaam kweli na nyie mtamnyima Magufuli kura?

Kwa bahati nzuri ninaishi maeneo matatu Tanzania.
Kote nimeona mabadiliko sio ya jiwe la msingi halafu hationi mwisho wake bali tunakuja kuona uzinduzi rasm.
Tunaoshinda mitandaoni kwa siku hatuzidi 100K.hivyo hizi danganya danganya zenu uchwara hazifiki popote,kati ya hiyo 100K.ni 3 K ndio ya ninyi wadanganyifu.
5 tena kwa JPM tuone uzinduzi wa miradi mikubwa nyie leteni mawazo kama ni mazuri yatatekelezwa.
 
Wana JF habari. Mi sio mwanasiasa Ila Uchaguzi tunaoshiriki ni wengi japokuwa wengine huwa hawapigi kura Ila maneno wanayo mengi kwenye vijiwe.

Kuelekea tarehe 28.10.2020 siku ya jambo la watu Fulani.
Bado najiluliza Kama wana Dar es Salaam nao watashindwa kumpa kura JPM..

Tunatambua wale jamaa wa Buhaya wao hawana masihara kabisa hapati kitu pale mheshimiwa .

Ila sasa kwa wana Dar es Salaam habari katika television zetu zilipambwa kwa kiasi kikubwa na maendeleo ya mkoa huo.

1.SGR(Railway)
2.Mbezi Stand
3.Ubungo FlyOver
4.Kinyerezi
5.The Port
6.Airport

Na mengine mengi ni heri wana Kaskazini wamnyime Ila sio wana Dar..

Ila ngoja tuone wana DSM wanalichukuliaje hili?
Sisi wananchi wa Jimbo la uchaguzi KAWE, kata ya Msasani ambayo in mitaa ya Masaki, Oyster Bay, Makangira, Bonde la Mpunga na Mikoroshoni, kura zetu tutampa Tundu Lissu kwa kiti Cha Uraisi, huyu ni CHADEMA. Ubunge tutampa Halima Mdee a.k.a Mama Lao, Mama la chuma cha pua kutoka CHADEMA. Na ubunge tutampa Luca Neghesti, mume wa Nancy Sumari, wa CCM.
 
Mtu wa Kwa Mpalange daraja la Coco Beach linamsaidia Nini? Acha sisi watu wa jimbo la KAWE na wale wa Kinondoni tulifaidi.
Watu wa Temeke watakuwa wanakuja weekend na mabangi yao kulishangaaa ila halitawanufaisha chochote
 
Vile Magufuli anajiandaa kwenda kwenye kampeni kuchamba wanawake
347890.jpg
 
Miradi hiyo yote siyo yake isipokuwa SGR tu. Ni miradi ya JK. Hana chake Dar.
Dar inataka haki, uhuru na maendeleo pia.
SGR siyo ya Magufuli ni ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na ile iliyoanzia Mombasa ambayo kwa Kenya karibu ikamilike lakini upande wetu imecheleweshwa na Magufuli kwa kutoamua haraka kuanza ujenzi. Nchi nne za Jumuiya zilipoona Tanzania na Burundi zinasuasua kuanza, ziliamua kuanza ujenzi peke yao na kuanzisha Umoja wao wa: "Coalition of the Willing" maana yake: "Umoja wa Waliotayari". Mradi huo ni toka wakati JK ikiwa ni pamoja na barabara ya Arusha Bypass ambayo imekamilika na Arusha - Voi ambayo Jiwe la Msingi limekwisha wekwa miaka kadhaa sasa na Kenyatta na Magufuli mpenda kuweka mawe ya msingi lakini utekelezaji hakuna. Barabara nyingine muhimu ya Jumuiya ambayo Jiwe la Msingi limewekwa lakini bado kuanza ni ile ya Tanga mpaka Bagamoyo kupitia Pangani ambayo ikikamilika itaunganisha Mombasa na Dar es Salaam bila kupitia Korogwe na Chalinze kama sasa. Wakazi wa Dar wafurahie madege tu.
 
Jiji la dar Lina idadi kubwa wahitimu wasiokuwa na ajira kuna watumishi wengi wasio ongezewa mishahara kwa kipindi cha miaka mitano wafanyabiashara na madalali vyuma vimekaza
Unazani umeona pale kwa mkapa watu wanavyotoka kuonesha dharau kwa kiongozi
 
Meko atachaguliwa na akina Chakubanga na Bashiru. Hakuna mnyonge atakayethubutu kumchagua dhalimu na dikteta asiyejali ustawi wa raia anaowaongoza.
 
Dar es salaam safari hii Magufuli atapata kura nyingi mno kutoka maeneo ya uswahilini ambako kuna wapiga kura wengi mno

Uswahilini kulikuwa kumesahauliwa Siku nyingi kwa miradi ya barabara za lami na umeme

Umeme wa uhakika utampa kura nyingi mno Magufuli Dar es salaam
Hakuna watumia umeme wengi kama watu wa Dar katika vitu wanaishukuru serikali ya awamu hii ni umeme wa uhakika
 
Wana JF habari. Mi sio mwanasiasa Ila Uchaguzi tunaoshiriki ni wengi japokuwa wengine huwa hawapigi kura Ila maneno wanayo mengi kwenye vijiwe.

Kuelekea tarehe 28.10.2020 siku ya jambo la watu Fulani.
Bado najiluliza Kama wana Dar es Salaam nao watashindwa kumpa kura JPM..

Tunatambua wale jamaa wa Buhaya wao hawana masihara kabisa hapati kitu pale mheshimiwa .

Ila sasa kwa wana Dar es Salaam habari katika television zetu zilipambwa kwa kiasi kikubwa na maendeleo ya mkoa huo.

1.SGR(Railway)
2.Mbezi Stand
3.Ubungo FlyOver
4.Kinyerezi
5.The Port
6.Airport

Na mengine mengi ni heri wana Kaskazini wamnyime Ila sio wana Dar..

Ila ngoja tuone wana DSM wanalichukuliaje hili?
Hawana ugali ndanu ya nyumba fly over haitasaidia
 
Magufuli hategemei kura za wananchi, kura zake za ushindi zipo Jamana Printers.
Hilo ndo linaloenda kutokea hiyo 2810.mateso yote waliyopata wapinzani kwa miaka mitano ilikuwa ni kulipiza,maana 2015 alipigwa na zezeta Ngoyai kura nyingi tu.Lubuva akafanya yake.

Moyoni aliumia sana ndo maana kwa miaka mitano akawa mkatili,kwa sababu wananchi walio wengi walichagua upinzani.

Sasa mwaka huu atapigwa chini kwa kura nyingi sana na Lisu,kitakachofanyika wajeda wataokoa jahazi arudi ikulu.
Miaka mitano inayokuja akiwa madarakani,hayo mateeso tutakayopata sio ya dunia hii,kwanza atakuwa hana hela za kumalizia miradi yake aliyoanzisha,maana uchumi umeshuka juu ya janga LA corona.
Yangu ni hayo.
 
Duh! Je hii nayo ni sera ya CCM? Kwamba kama wananchi wanataka shule zao ziboreshwe wasubiri tetemeko liwakumbe, kama wanataka miundo mbinu iboreshwe wasubiri tetemeko liwakumbe...Hizi ni akili za wapi?
Wewe ndio unaendekeza akili mbovu. Kila siku kipindi hiki cha kampeni zinatajwa idadi ya shule zilizokarabatiwa ambazo zilishageuka magofu na ni nyingi.

Elewa hoja ya mtu kabla hujadandia treni kwa mbele.
 
Hata Buhaya watampa kura nyingi tu. Pesa za tetemeko zimeboresha shule ya sekondari imekuwa ya kisasa na kuna meli zipo ziwa Victoria zinafanya kazi nzuri.

Watu wa Dar hatuna sababu ya msingi ya kumkataa Magufuli, tuna sababu ya kuwakataa wabunge wanaokwenda bungeni kuvaa vitambaa midomoni na kutoka nje ya ukumbi wakiwa wameshachukua posho ya siku.
Na wale wa ndiyooooooo kwa kila kitu ndo WA kuwachagua?
 
Mkuu zile pesa ndio lilikuwa lengo lake?
Alafu si vizuri kuwaongelea wakazi wa Dar wote kuwa tutampigia kura jiwe wakati hapa ndio kitovu cha wasomi, waelewa wa mambo yanavyoenda. Kingine ukisema hivyo manaake ni kuwa wanaDar wote tunakubaliana na uminywaji wa uhuru na haki za binadamu, kwamba tulifurahia makonda alivyoingia na askari wa usalama wa taifa pale Clouds Tv wakiwa na silaha za kivita, tunakubaliana na kupotea kwa Ben Saanane na vile viroba vya maiti kwenye fukwe za bahari ya Hindi Dar..
Wanadar hawadanganyiki na uboreshwaji wa miundombinu kwasababu huo ni wajibu wa serikali maana inatumia pesa zetu. Tar 28 ni siku nzito na kila mtu ana jambo lake
Hao wanadar wenye mbwembwe za usomi siku zote kwenye masuala ya uchaguzi hawasumbui.

Siku zote wapo wasomi wengi wenye kutafakari mambo kwa kina na wapo wale wasomi wa Bar wazee wa pinga pinga na mara nyingi hawa huwa hawaendi hata kupiga kura.
 
Back
Top Bottom