Mkuu zile pesa ndio lilikuwa lengo lake?
Alafu si vizuri kuwaongelea wakazi wa Dar wote kuwa tutampigia kura jiwe wakati hapa ndio kitovu cha wasomi, waelewa wa mambo yanavyoenda. Kingine ukisema hivyo manaake ni kuwa wanaDar wote tunakubaliana na uminywaji wa uhuru na haki za binadamu, kwamba tulifurahia makonda alivyoingia na askari wa usalama wa taifa pale Clouds Tv wakiwa na silaha za kivita, tunakubaliana na kupotea kwa Ben Saanane na vile viroba vya maiti kwenye fukwe za bahari ya Hindi Dar..
Wanadar hawadanganyiki na uboreshwaji wa miundombinu kwasababu huo ni wajibu wa serikali maana inatumia pesa zetu. Tar 28 ni siku nzito na kila mtu ana jambo lake