Katika mikoa iliyoathirika na serikali ya awamu ya tano ni Dar es salaam. Kuhamisha makao makuu ya nchi kwenda Dodoma ni pigo la historia kwa wakazi wa Dar es salaam. Balozi zote zitaamua Dodoma,ikulu Dodoma,wizara zote Dodoma, mashirika ya kimataifa Dodoma, mashirika ya umma Dodoma,wafanyakazi wote Dodoma,uwanja wa ndege wa msalato Dodoma. Sasa akawadanganya kuondoa foleni dar kwa kujenga flyover,sio kweli kwanza foleni dar haitakuwepo kwani serikali inaondoka kwenda Dodoma. Kwa mantiki hiyo uchumi wa dar ikifika mwaka 2025 wananchi wengi watakuwa omba omba kwani miradi yao mingi itakuwa imekufa au haipo tena.
Magufuli amehamishiwa makao makuu Dodoma kwa makusudi kwa kutambua kuwa watu wengi waliiba fedha serikalini awamu zilizopita na kuwekeza Dar,Sasa walioiba washindwe kuwekeza Dodoma na miradi iliyopo dar ife. Kwa kifupi Dar hali itakuwa mbaya sana .tunadanganywa dar itakuwa jiji la biashara biashara ipi itajwe? Utawala huu utaacha historia dar kuweni nao makini sana.