Wakazi wa Dar: Tahadhari, epuka njia hii usiku huu

Kama haujui jeshi halina rafiki wa kudumu mwambieni aendelee kuwamwaga mtaani.
Alafu mtaona KIFUATACHO.mwambieni AENDELEE kuwaruhusu waingie mitaani.
Ningekujibu lakini ID yako inajitosheleza
 
Wee kiazi kweli kama ilikuwa hali ya kawaida si tungekuwa tushaizoea?
 
Jiji zima usiku wa leo limetawaliwa na hao watu, hakuna uhuru na amani kabisa.
Uhuru gani unaoutaka, ? Amani gani unayoitaka.? Kama sio muarifu unawasiwasi gani...? Majeshi yetu Yapo kwa mujibu wa sheria, Na kazi ya jeshi nikulinda Amani na mipaka yetu haswa katika kipindi kigumu Kama Hiki cha uchaguzi.... Ulitaka watu wausalama walale nyumbani ! Ili wewe udhulule usiku ndiyo amani na uhuru unaoutaka...? hivi yanayoendelea NIGERIA unayaona au huyaoni....! Kama wewe sio mualifu na hauvunji sheria za nchi Basi hupaswi Kua na Hata chembe ya uoga..... Majeshi ya ulinzi na salama wapo hapo na kwengineko kwa ajili yako na usalama wa wa TANZANIA wote. Tii sheria Bila shurti wala hauto shurutishwa.
 
Kweli kabisa mkuu, mtoa Mada hajielewi
 
Hao jamaa niliwaona Changanyikeni jana na Kalandinga lao nikasepa kijiweni kuepuka fedhea.
 
#Mtoasirikificho: Badala ya kuwapongeza hawa wanajeshi wanasaidia kuzuia uharifu lakini wewe unwashitua watu wenye nia ovu wapite maeneo mengine!!! Hii inashangaza kama kweli ni Mtanzania basi kuna tatizo mahali ambapo inawezekana wewe ni sehemu ya mnyororo wa waharifu. Kama wewe huna tatizo lolote kwanini uwe na hofu? Wanajeshi tumewaajiri sis Watanzania kuhakikisha nchi ni salama wewe unlalamika kuwaona wako kazini tena katika eneo unalopita. Inawezekana huna ufahamu fasaha wa kazi za askari jeshi hasa nyakati za uchaguzi na kukawa na viashiria vya uharifu wa kuvuka mipaka.
 
Noted
 
baba wa Taifa Nyerere angekuwa na akili kama zako ungekuta bado tupo utumwani
 
Yaani kuhojiwa kidogo tu tayari umeona usumbufu ila ukikuta waliofunga njia ni maninja hata sura huwaoni na wanatumia magogo kama road block alafu ni usiku sijui utasemaje. Kiuhalisia hio njia ipo eneo la kambini kwahio usisangae mara nyingi sana wakat taifa lipo kwenye tension ulinzi unatakiwa uwe kwenye kiwango kisicho na mashaka.
 
Utakuwa umewaonyesha kadi yako ya CCM. Ni wazi Mabeyo kawaambia nyie wasiwasumbue.
 
Tatizo la wanajeshi kusipokuwa na vita wanatafuta adui kwa nguvu. Hapa Tanzania siku hizi kuwa mwanajeshi ni sawa na kuwa kula kulala tu, kwa hiyo wanaziona hizi kama fursa, kusumbua watu
 
Hadith za Kilaza Hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…