Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Wakazi wa mji wa Bukavu uliyoko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokraisia ya Congo wamesema kuhukumiwa kifo kwa rais wa zamani, Joseph kabila, hakutaleta amani ambayo wanatamani, ila itaongeza hali ya mvutano. Bukavu ilivamiwa na waasi wa M23 tangu Februari 2025.
Mahakama ya Kijeshi nchini DRC ilimtia hatiani Kabila kwa madai ya uhalifu wa kivita, uhaini, na uhalifu dhidi ya binadamu, huku akituhumiwa kuunga mkono kikundi cha waasi cha M23..