Taifa Digital Forum
Member
- Jun 4, 2022
- 68
- 184
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Mhe. Dkt Pindi Chana akiwakaribisha wananchi waliohama kwa Hiari kupisha shughuli za uhifadhi katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Leo Juni 16, 2022 Kaya takribani 20 zimewasili katika kijiji cha Msomera kilichopo Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga eneo lililotengwa na Serikali.
=====
MAWAZIRI, Innocent Bashungwa (Tamisemi), Balozi Pindi Chana (Maliasili na Utalii na Utalii), Jumaa Aweso (Maji), na Naibu Waziri Ridhiwani Kikwete wamejumuika kupokea kaya 20 kati ya 290 zilizowasili Msomera, Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga baada ya kuamua kuondoka kwa hiyari katika eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Kaya hizo zimewasili kwa kusafirishwa na Serikali ikiwa ni awamu ya kwanza na kuanza makazi mapya katika eneo la Msomera ili kupisha shughuli za uhifadhi katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.
Waziri Bashungwa amesema, tayari Serikali imeweka mazingira mazuri kwa ajili yao ambapo Serikali ilileta Sh milioni 400 kujenga shule mpya za msingi na sekondari na bweni moja katika Kata ya Misima ndani ya Kijiji cha Msomera ambazo zimekamilika ili wanafunzi wasitembee mwendo mrefu kupata masomo ya elimu ya msingi na sekondari.
Serikali imetoa Sh milioni 500 kuanza ujenzi wa kituo cha afya Msomera ambao unaendelea na Sh milioni 50 kwa ajili ya kupanua na kuboresha huduma za afya katika zahanati ya Kijiji cha Msomera katika kata ya Misima Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga kinachotoa huduma kwa wananchi wasiopungua 10,000.