Wakazi wa Itumbi Chunya tunahitaji lami

Wakazi wa Itumbi Chunya tunahitaji lami

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Migodi ya wachimbaji wadogo wa dhahabu Itumbi Chunya Mbeya ni mingi zaidi ya wachimbaji wadogo na kati 5000 tupo eneo hili, ila tuna changamoto kubwa ya kukosekana kwa barabara ya lami.

Tafadhali serikali mtuwekee lami huku ili biashara yetu ya madini iwe rahisi. Tunazalisha sana madini huku ila kukosa lami kunatukosesha fursa nyingi na kukwaza maendeleo ya sekta hii.

Pia tunaomba mawasiliano ya simu huku yako duni sana hatupati mitandao pendwa hapa Itumbi hasa VODACOM AIRTEL NA TIGO...Halotel yupo kwa mbali lakini kwa mashaka.......hapa pamoja na familia zetu tupo zaidi ya watu 20,000 kutopata mawasiliano ya uhakika sio sawa.
20210824_183034.jpg
20210824_183038.jpg
 
Ivi hata umeme wa TANESCO walikwisha weka?
Itumbi kwa sasa ni kuchele kwa maendeleo ya watu binafsi, tatizo serikali imeipa kisogo eneo husika ktk suala zima la uwekezaji wa kimaendeleo.
 
Mwambalaswa anasemaje?
Alafu mleta post anasema wajimbaji wapo zaidi ya 5,000/ wangeanzisha tozo ya 20,000/kila mwezi ndani ya miaka 5 wangeweka Lami,
Lakini mkimtegemea mbunge wenu aliyepitishwa na mfumo mtazeeka.
 
Ivi hata umeme wa TANESCO walikwisha weka?
Itumbi kwa sasa ni kuchele kwa maendeleo ya watu binafsi, tatizo serikali imeipa kisogo eneo husika ktk suala zima la uwekezaji wa kimaendeleo.
Umeme bado ila ndo wanamalizia kutuwekea nguzo labda utawaka hivi karibuni kero kubwa huku kwa sasa ni barabara na hiki kipande hadi Matundasi sio kirefu sana...watuletee barabara tunalima dhahabu ya kutosha sana huku zaidi ya kilo 300 kila mwezi tunatoa huku ila ndo barabara tumesahaulika
 
Alafu mleta post anasema wajimbaji wapo zaidi ya 5,000/ wangeanzisha tozo ya 20,000/kila mwezi ndani ya miaka 5 wangeweka Lami,
Lakini mkimtegemea mbunge wenu aliyepitishwa na mfumo mtazeeka.
Kazi ya kuweka lami ni ya serikali ndiyo inayoratibu....sisi tayari tunalipa fedha za huo ujenzi kwa kulipa kodi tena ya kutosha na tuna ofisi ya madini huku na Kamishna wa madini huku...na Chunya ni Mkoa maalum wa kimadini...kwanini tujichangishe mara mbili wakati kodi tayari tunatoa!?...TUNATAKA BARABARA YA LAMI ITUMBI CHUNYA.
 
Mkuu tusubiri kwanza barabara ya kutoka Mbalizi,mkwajuni mpaka saza kwanza halafu tutaiangalia na hiyo
 
Kazi ya kuweka lami ni ya serikali ndiyo inayoratibu....sisi tayari tunalipa fedha za huo ujenzi kwa kulipa kodi tena ya kutosha na tuna ofisi ya madini huku na Kamishna wa madini huku...na Chunya ni Mkoa maalum wa kimadini...kwanini tujichangishe mara mbili wakati kodi tayari tunatoa!?...TUNATAKA BARABARA YA LAMI ITUMBI CHUNYA.
Siyo Serikali tu maendeleo na ujenzi wa Taifa letu linahitaji ushirikiano Kati ya Serikali na wananchi,ndiyo maana wangeanzisha Tozo kwenye Petrol na huduma za kifedha bila kushilikishwa, ili fedhha zinazopatikana ziede kujenga vyumba vya madalasa na vituo vya Afya.

Onyesheni uzalendo kwa kuanzisha tozo yenu,vinginevyo mnaweza kusubili sana.
 
Kwani lami mliyowekewa kwenu wanakijiji mlichangishana?
Na kama bado hamjawekewa lami, mnasubiri nini kuchangishana?
Kazi ya kodi za serikali ni kwa ajili ya matumizi gani?
Katiba inasemaje juu ya usawa wa kimaendeleo kwa wanachi wake?
 
Mkuu subiri kidogo huku kigamboni kuanzia cheka Mpaka Buyuni hamna lami.Mzee wa vifurushi kapotea Mazima.Nyangasa kapwaya Sana. Alitakiwa aombe mwendo Kasi Kigamboni inakua kwa Kasi
 
Umeme bado ila ndo wanamalizia kutuwekea nguzo labda utawaka hivi karibuni kero kubwa huku kwa sasa ni barabara na hiki kipande hadi Matundasi sio kirefu sana...watuletee barabara tunalima dhahabu ya kutosha sana huku zaidi ya kilo 300 kila mwezi tunatoa huku ila ndo barabara tumesahaulika
Itumbi ilistahili kupatiwa umeme wa TANESCO tangu miaka 15 iliyopita.
Wamechelewesha sana, hicho kijiji kingekuwa mbali sana kimaendeleo sasa ivi.
 
Itumbi nimefika, watu binafsi wamejitahidi sana kupaendeleza. Mahitaji muhimu yapo na kila aina ya biashara ipo utadhani upo Mwanjelwa. Wana Itumbi wakipatiwa huduma muhimu za kijamii wanaweza kuipiku Matundasi au hata Makongolosi.

Vuteni subira maana kwa Tanzania wanatangulia watu kuishi mahali, maendeleo yanawafuata baadaye. Ilipaswa yatangulie maendeleo ya huduma za msingi, hasa miundombinu ndipo waingie watu.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Migodi ya wachimbaji wadogo wa dhahabu Itumbi Chunya Mbeya ni mingi zaidi ya wachimbaji wadogo na kati 5000 tupo eneo hili, ila tuna changamoto kubwa ya kukosekana kwa barabara ya lami.

Tafadhali serikali mtuwekee lami huku ili biashara yetu ya madini iwe rahisi. Tunazalisha sana madini huku ila kukosa lami kunatukosesha fursa nyingi na kukwaza maendeleo ya sekta hii.

Pia tunaomba mawasiliano ya simu huku yako duni sana hatupati mitandao pendwa hapa Itumbi hasa VODACOM AIRTEL NA TIGO...Halotel yupo kwa mbali lakini kwa mashaka.......hapa pamoja na familia zetu tupo zaidi ya watu 20,000 kutopata mawasiliano ya uhakika sio sawa. View attachment 1906853View attachment 1906854
Nunueni magari mazuri na sio Bedford na iPhone ndipo muwekewe lami
 
Back
Top Bottom