Huyo ni mfadhiri wa CCM, msimletee bugha!Mh Mkuu wa wilaya na mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Pwani najua huko kwenu mnalala usingizi ila sisi wana makurunge hatulali kutokana ka kelele za mitetemo kutoka kwenye bar ya REDOMAX.
Tuna wagonjwa , wengine tunelitumikia taifa wiki nzima na tunahitaji akili yetu ipumzike ili Jumatatu tukasukume gurudumu la maendeleo lakini ndio hatuwezi sasa kila siku ni kelele, hapa nilipo ni karibu mita 500 kutoka bara ilipo ila siwezi kulala kabisa ,tuambiwe tatizo nini au mmeshindwa kazi kuombe msaada ngazi za juu zaidi .
Nafahamu kuna taratibu za kuzuia kelele na mtetemo hasa kiujenzi ambapo sauti hubakia ndani sio kwenye open bar kama ile .
Kwa niaba ya wakazi wa makurungu majumba sita tunaomba ulifanyie kazi jambo hili
USSR
usipokuwa mwangalifu hata hicho kibanda unamoishi (kwa kupanga chumba) Samia atatoa amri kivunjwe; kuliko kuingilia shughuli za watu waliomweka madarakani na kumlinda usalama wake.
Kwa mtu kama wewe, nami nawahimiza waongeze mitetemo zaidi, labda akili ndio zitawaingia kichwani.