Wakazi wa Kipunguni Dar es Salaam ambao tuliteseka zaidi ya miaka 20 mwaka huu tumefanyiwa tathimini ya majengo na ardhi. Tunasubiri malipo

Wakazi wa Kipunguni Dar es Salaam ambao tuliteseka zaidi ya miaka 20 mwaka huu tumefanyiwa tathimini ya majengo na ardhi. Tunasubiri malipo

Joined
Apr 1, 2023
Posts
12
Reaction score
9
Mheshimiwa Rais mama yetu mpendwa. Wakazi wa Kipunguni Dar salaam ambao tuliteseka Zaid ya miaka 20 mwaka huu tumefanyiwa tathimini ya majengo na ardhi. Tunasubiri malipo.

Lakini tunaona siasa zimeanza maana mpaka Sasa bado hatujajua lini tutalipwa. Ingawa mmbunge wetu Segerea Bona Kimori akiendelea kutupigania.

Lakini SERIKARI haitaki kusema inatulipa lini. Tunateseka ktk Nchi yetu. Tunaomba msaada wako. Hapo useme kitu watakusikia asante
 
Mbunge Bonah Kamoli tunaomba ufafanuzi juu ya suala la bomoa Bomoa Kipunguni, ikiwezekana kikao itakuwa vyema zaidi, maana hakueleweki maana tunasikia ni mwezi wa nane mara mwezi wa Saba. Unafahamu fika juu ya adha inayo tukabiri wakazi wa Kipunguni.

Tunaomba kujuzwa. Tunajua unatupambania lakini tunaomba kikao na wewe tunaomba tukuone uje utuletee hao Mawaziri husika kwenye kikao haraka maana muda ukiisha usije kutubembeleza kisiasa, utakuwa adui wetu namba moja.

Tunaomba tupate majibu ya ujumbe huu haraka.
 
Nakaa Kipunguni B. Bomoaboa hiyo iko sehemu gani?
KIPUNGUNI (A) na Kipunguni mashariki ambayo unaingilia Banana tumepakana na uwanja wa ndege. Tuna mgogoro miaka 22 Sasa . Mwaka huu wametufanyia tathimini lakini SERIKALI hawasemi ukweli wanatulipa lini Yaani hii SERIKALI yetu haiwajali wananchi wake kabisa
 
Hili suala la bomoa bomoa kipunguni A,linanigusa sana.Nyumba yetu iliwekewa alama na namba ya nyumba mwaka 1996, na kusitisha uendelezaji wa ujenz na makazi eneo la kipunguni A.
 
Wapelekwe mahakamani.Tatizo ni TAA hawasemi ukweli. Something fishy.
 
Sijajua serikali INA mpango gani, kwasababu toka tathmini ifanyike ikipita miezi sits hawajalipa itabidi tathmini ifanyike upya hiyo ni kisheria, lakini hakuna taarifa yoyote unayotolewa na muda unazidi kwenda, hii project imekaa kigizagiza sana na wakirudia tathmini ni hasara kwa serikali kutumia pesa Mara tatu kwa jambo moja.
 
Mimi ninafikiri tayari miezi sita imepita serikali inapaswa ifanye tathmini upya. Waziri wa ujenzi na uchukuzi anasemaje, Mbunge naye ameonekana kuwadanganya wananchi wa jimbo lake, jimbo hili litaenda upinzani wasipoangalia.

Kama wako makini waendelee na hatua ya kuingia mikataba ya malipo"vendor agreement" na kufanya malipo badala ya visingizio mbalimbali kuvuta muda.

Wataiingizia Serikali hasara kubwa baadaye wasipofanya hivyo. Hapa hakuna ujanja.

Kipunguni A wajipange kumuona Waziri wa ujenzi na uchukuzi, ikishindikana Mh Rais au sheria ichukue mkondo wake mahakamani ili watu waendeleze makazi yao.
 
Sijajua serikali INA mpango gani, kwasababu toka tathmini ifanyike ikipita miezi sits hawajalipa itabidi tathmini ifanyike upya hiyo ni kisheria, lakini hakuna taarifa yoyote unayotolewa na muda unazidi kwenda, hii project imekaa kigizagiza sana na wakirudia tathmini ni hasara kwa serikali kutumia pesa Mara tatu kwa jambo moja.
Nawaombeni mjiandae kisaikolojia, mtalia na kusaga meno.Waulizeni bonde la mto Msimbazi!!!!!!!!! Nyumba ya milioni 40 unapewa milioni 3!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Hoja: Siyo eneo la makazi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Unajua ilikuwa lini hiyo!!!!!!!!!!!!! 1970s( miaka ya 1970)

Ushauri: Fuatilia eneo lenu mnaweza kuambiwa kuwa mmevamia ardhi!!!!!!!!!!!!!!

Nb: Mto msimbazi walipelekewa huduma zote za kijamii na haohao serikali licha ya kusema kisheria siyo eneo la makazi!!!!!!!!!!!! Usije ukapaza shingo eti mbona umeme,maji,shule, walituletea!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kuna watu wana hati za ardhi makazi"certificate of occupancy"zilizotolewa na mamlaka kihalali, na hivyo mjadala unaouanzisha sidhani kama una mashiko.

Ina maana tathmini ilyofanyika na watu kusaini tathimini ni magumashi, nadhani kama kuna shida ya pesa ya kulipa liwekwe wazi tu,lakini ninaamini tathmini ilipofanyika bajeti ilikuwepo au kuna sababu ya mchakato wa kufuta hati za ardhi za baadhi kabla ya malipo?

Hatua ya mikataba"vendor agreement" na malipo ndiyo iliyobaki(iliyosalia pending) kuanzia machi 2023. Suala la msimbazi ni tofauti na Kipunguni A.

Kuna watu walikwisha lipwa eneo hilo hilo la Kipunguni A huko nyuma kwa tathmini ya 1996 wengine wakawa hawakulipwa,ni mwendelezo wa zoezi, tathmini ikarudiwa 2022/23, hakuna double standard hapo ya kimsimbazi.

Je walilipwa kimakosa watu hao,basi wawajibike watendaji wa TAA km itakuwa hivyo.
 
Back
Top Bottom