A
Anonymous
Guest
Wakuu, habari.
Ninaomba kufikisha kilio cha wananchi wa maeneo ya Kitunda, Kibeberu, Magole (Mzinga/Kivule) kuhusu changamoto kubwa ya ukosefu wa viwanja vya michezo vya jamii, hususan kwa vijana wanaopenda mpira wa miguu.
Mimi ni mkazi wa eneo hilo. Changamoto hii imekuwa ikiathiri sana maendeleo ya vipaji vya vijana, kwani maeneo mengi yanayotumika kuchezea ni ya shule au taasisi binafsi, na siyo viwanja vya wazi vya jamii.
Kwa mfano, vijana wa Kitunda hutegemea kiwanja cha shule ya Kitunda, ambacho hupatikana kwa masharti ya kuomba kibali kwa uongozi wa shule. Hali kama hiyo pia ipo Tumaini ambapo eneo linatajwa kuwa la soko na zahanati, hivyo matumizi ya kuchezea mpira ni ya muda na yanaweza kusitishwa wakati wowote.
Kibeberu nako kuna kiwanja kilicho katika mgogoro, wakati Magole wanategemea kiwanja cha shule ya Magole, na Mwanagati hutumia viwanja vya shule na makanisa ambavyo pia vina masharti ya matumizi na mara nyingine hufungiwa bila taarifa ya awali.
Changamoto hii imeathiri timu nyingi za vijana, ikiwemo academy zinazofundisha watoto wa umri tofauti kama under 12 na under 17, pamoja na timu za wasichana zinazoshiriki mashindano mbalimbali.
Wananchi wanasema kukosekana kwa viwanja vya jamii vya viwango vya kawaida kunasababisha kupotea kwa vipaji, kuongezeka kwa mmomonyoko wa maadili, na hata kupunguza fursa za vijana kujiajiri kupitia michezo.
Wanaomba mamlaka husika, hususan Wizara ya Michezo na Serikali za Mitaa, kuingilia kati kwa kuandaa na kuboresha viwanja vya wazi vya jamii, ikiwemo kusawazisha na kuboresha baadhi ya maeneo ya shule ili yaweze kutumika kwa muda maalum kwa jamii.
Lengo ni kuhakikisha vijana wanapata sehemu salama na rasmi ya kufanya mazoezi, kukuza vipaji, na pia kusaidia jamii kupata sehemu za burudani na afya kupitia michezo.