A
Anonymous
Guest
Wakazi wa Malamba Mawili kwa Ndodi, Mtaa wa Chande B, Dar es Salaam kuna jengo la ibada linaitwa King'azi B Kisima cha Sifa, bila kuwakosea heshima wahusika lakini kwa kweli limekuwa kero kwa Wananchi, kutokana na wahusika kupiga muziki kwa nguvu sana mpaka usiku wa manane.
Sauti kubwa sana kiasi kwamba hakuna masikilizano, tunajua wanafanya hivyo kama njia ya mumtukuza Mungu au kufanya ibada n.k lakini tumejaribu kuwaomba mara nyingi kupunguza sauti, kinachotokea ni kuwa hawatusikilizi, tumeenda Serikali za Mitaa napo hakuna majibu ya kueleweka.
Vijana wachache unawakuta wanapiga muziki hasa tena kwa sauti ya juu mnoo hii inatuathiri wakazi tuna watoto wadogo, wagonjwa na wazee ambao wanaishia kuumia tu bila msaada tupazie sauti tafadhali.
Wahusika wao ni kupiga mziki tu hata ibada wanafanya muda mchache, NEMC mko wapi mje mtusaidie kuhusu hii kero.