Jana mida ya saa 5 usiku maeneo mbalimbali ya manispaa ya Morogoro wananchi waliokuwa wakisherekea mwaka mpya walipigwa na polisi kwa kuonekana barabara au baa kuanzia saa 5 usiku kabla hata ya mwaka mpya 2020 kufika.
Gari 2 za polisi wakiwa na mbwa zilizunguka maeneo mbali mbali ya manispaa ya Morogoro ikiwemo Mazimbu Road, mtaa wa Kwawagogo na Lukobe kutaja kwa uchache na kuwatandika makofi, fimbo ikiwa pamoja na kuwafunga pingu watu waliokuwa wakihoji sababu za kupigwa.
Polisi pia walivamia ndani ya baa wakawatandika viboko wahudumu wa baa, wateja pamoja na kumwaga bia walizozikuta mezani.
Wananchi wanahoji mbona hakukuwa na taarifa ya tahadhari ya kutoruhusiwa, au katazo la kusherekea Mwaka Mpya maeneo hayo iliyotolewa kabla?