Sisi wakazi wa maeneo ya Kimara kwa Msuguli, Kibanda cha Mkaa, Mbezi Mwisho Kwa Yusuph, na Mbezi Mazulu tunakumbwa na changamoto kubwa ya maji machafu kutoka kwenye mabomba.
Kwa takribani wiki mbili sasa, tumekuwa tukipata maji yenye tope badala ya maji safi na salama.
Hali hii ni hatari kwa afya zetu kwani maji haya yanaweza kusababisha magonjwa ya tumbo, ngozi na hata maambukizi mengine ya bakteria.
Tunaiomba mamlaka husika (DAWASA au wahusika wa usambazaji wa maji) kuchukua hatua za haraka kutatua tatizo hili na kuhakikisha tunapata maji safi na salama kwa matumizi ya nyumbani.
Tunaomba mamlaka zitupatie taarifa rasmi kuhusu chanzo cha tatizo hili na hatua zinazochukuliwa ili kurejesha huduma ya maji safi kwa wakazi wa maeneo haya.