KERO Wakazi wa Mwanza eneo la Isamilo hatuna maji takriban wiki nzima, Serikali iangalie suala hili kwa umakini

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Joined
Sep 28, 2024
Posts
66
Reaction score
46
Samahani kwa usumbufu utakaotokea, ila nina jambo la moyoni ambalo nahitaji kulitoa. Kwangu mimi na kwa jamii inayonizunguka, limekuwa likitusumbua sana. Ni kwamba hatuna pa kusemea matatizo yetu moja kwa moja, lakini namshukuru Mwenyezi Mungu kwa uwepo wa mtandao huu pendwa wa jamii, unaosikiliza, kuchambua, kulinda, kuwasilisha, na kujali changamoto zote zinazowasilishwa hapa JF.

Mimi ni mdau na Mtanzania halisi. Kwa sasa tunapata shida kubwa sana upande wa huduma ya maji. Takribani wiki nzima sasa, maji yamekuwa tatizo kubwa ndani ya Jiji la Mwanza, hususan upande wa Isamilo.

Hali hii imekuwa tishio na ni hatari hasa kwa mama zetu, dada zetu, na watoto, maana inawalazimu kuamka usiku sana ili kuwahi foleni ya maji wasije wakakosa. Kwa wamiliki wa matenki, hali hii pia inaleta changamoto kubwa kwa wananchi.

Wito wangu ni kwa Serikali yetu kuangalia kwa makini suala hili, ili kuzuia changamoto kubwa zaidi za baadaye na kuhakikisha mahitaji ya maji kwa wote yanapatikana bila kero.

Ni wenu katika ujenzi wa taifa,
Kimwaga Campus
1000147520.jpg
 
Mwanza kukosa maji wakati Ziwa Victoria lipo hapo tu ni aibu.
Alafu hapo Isamilo ziwa unaliona tu kwa macho, watu wa kahama na Shinyanga wanapata maji 24hrs daily toka ziwa Victoria huku maeneo mengi ya Mwanza maji ni kwa mgao au hayapatikani kabisa. Hii nchi ina vituko vingi
 
Ishu ya maji imekuwa kero hapa Mwanza ni takribani wiki nzima sasa maji yanatoka kwa kusua sua.
 
Siyo Isamilo tu ni Karibu maeneo yote ya jiji la Mwanza.Kuna jamaa mimeongea nae pale Igoma wanateseka pia na maji takribani wiki 2
 
Samahani kwa usumbufu utakaotokea, ila nina jambo la moyoni ambalo nahitaji kulitoa. Kwangu mimi na kwa jamii inayonizunguka, limekuwa likitusumbua sana. Ni kwamba hatuna pa kusemea matatizo yetu moja kwa moja, lakini namshukuru Mwenyezi Mungu kwa uwepo wa mtandao huu pendwa wa jamii, unaosikiliza, kuchambua, kulinda, kuwasilisha, na kujali changamoto zote zinazowasilishwa hapa JF.

Mimi ni mdau na Mtanzania halisi. Kwa sasa tunapata shida kubwa sana upande wa huduma ya maji. Takribani wiki nzima sasa, maji yamekuwa tatizo kubwa ndani ya Jiji la Mwanza, hususan upande wa Isamilo.

Hali hii imekuwa tishio na ni hatari hasa kwa mama zetu, dada zetu, na watoto, maana inawalazimu kuamka usiku sana ili kuwahi foleni ya maji wasije wakakosa. Kwa wamiliki wa matenki, hali hii pia inaleta changamoto kubwa kwa wananchi.

Wito wangu ni kwa Serikali yetu kuangalia kwa makini suala hili, ili kuzuia changamoto kubwa zaidi za baadaye na kuhakikisha mahitaji ya maji kwa wote yanapatikana bila kero.

Ni wenu katika ujenzi wa taifa,
Kimwaga Campus
View attachment 3442375
Huko hakuna Wabunge na Madiwani?
 
Kama Ziwa halijakauka,

Mna haki ya kupewa maji.

DC awaletee maji toka nyumbani kwake,maana yapo hayajakatwa
 
Mwanza kukosa maji wakati Ziwa Victoria lipo hapo tu ni aibu.
Ni kweli ziwa lipo Ila Mfumo Uliopo ndo kipengere. Kila Mjenzi Aliejaaliwa kumiliki Aridhi.
Kwa Kadari zake Allah.
Analo Bomba Ila Maji Hayatoki.
Je' Nani Atafungasha Safari.
Kwenda kuchota Maji ziwani.
Ili Hali Tulishaaminishwa Sio salama?
Mpaka Tuyapate Yale Yaliyo Andaliwa na Mfumo?
 
Alafu hapo Isamilo ziwa unaliona tu kwa macho, watu wa kahama na Shinyanga wanapata maji 24hrs daily toka ziwa Victoria huku maeneo mengi ya Mwanza maji ni kwa mgao au hayapatikani kabisa. Hii nchi ina vituko vingi
Hatuna Namna Tutazidi Kupiga Kerele Sana.
Hata wakiweka pamba masikioni.
Ila saut za wananchi zitapenya tu.
Bidhinllah
 
Vuteni subira waungwana
Tumieni kwa busara hayo yanayopatikana
Kweli Kuna Busara Ndani ya Kupambania Pumzi? Ukitaka Kuamini
Itokee Siku Lala nyumbani Kwako.
Ukiwa Huna Hata Tone La Maji.
Halafu Kutana Na Mtihani.
Wa Kuuguliwa Kama Hujaaenda Kukutana Nayo Hospital Na Ilihali mgonjwa mwenyewe.
Ulishampoteza Kwa Uzembe Wa Wachache.
 
Mwanza kukosa maji wakati Ziwa Victoria lipo hapo tu ni aibu.
Kukosa vipaumbele na mikakati kwa hii Serikali ndio Aibu kubwa mkuu, Miaka ya nyuma niliwahi kukutana na Mtumishi wa MWAUWASA mamlaka ya Maji hapo Mwanza , ilikuwa eneo la kazini nae alikuja kupata huduma tukamhoji sana akasema hivi vyanzo vya maji hapo Mwanza vilikuwa vya kuacomodate watu kama laki 8 tu na hakukuwa na kelele Miaka hiyo kwasasa Mwanza inawatu zaidi ya 2M na wanazid kuongezeka vyanzo ni vilevile kile kipya Cha Butimba alichozindua juzi Hangaya ni kidogo sana ni kama hakuna maajabu mradi wa 93B ni mdogo sana kwa Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela maeneo ya Pembezoni ni shida lazima ulie
 
Siyo Isamilo tu ni Karibu maeneo yote ya jiji la Mwanza.Kuna jamaa mimeongea nae pale Igoma wanateseka pia na maji takribani wiki 2
Maeneo yote ya Pembezoni na Jiji ni shida mkuu wanaofaidi ni waliopo kati kati na KM chache kutoka Chanzo kikuu cha Maji
 
Samahani kwa usumbufu utakaotokea, ila nina jambo la moyoni ambalo nahitaji kulitoa. Kwangu mimi na kwa jamii inayonizunguka, limekuwa likitusumbua sana. Ni kwamba hatuna pa kusemea matatizo yetu moja kwa moja, lakini namshukuru Mwenyezi Mungu kwa uwepo wa mtandao huu pendwa wa jamii, unaosikiliza, kuchambua, kulinda, kuwasilisha, na kujali changamoto zote zinazowasilishwa hapa JF.

Mimi ni mdau na Mtanzania halisi. Kwa sasa tunapata shida kubwa sana upande wa huduma ya maji. Takribani wiki nzima sasa, maji yamekuwa tatizo kubwa ndani ya Jiji la Mwanza, hususan upande wa Isamilo.

Hali hii imekuwa tishio na ni hatari hasa kwa mama zetu, dada zetu, na watoto, maana inawalazimu kuamka usiku sana ili kuwahi foleni ya maji wasije wakakosa. Kwa wamiliki wa matenki, hali hii pia inaleta changamoto kubwa kwa wananchi.

Wito wangu ni kwa Serikali yetu kuangalia kwa makini suala hili, ili kuzuia changamoto kubwa zaidi za baadaye na kuhakikisha mahitaji ya maji kwa wote yanapatikana bila kero.

Ni wenu katika ujenzi wa taifa,
Kimwaga Campus
View attachment 3442375
Isamilo ya 90s haikuwa hivi.
 
Back
Top Bottom