Samahani kwa usumbufu utakaotokea, ila nina jambo la moyoni ambalo nahitaji kulitoa. Kwangu mimi na kwa jamii inayonizunguka, limekuwa likitusumbua sana. Ni kwamba hatuna pa kusemea matatizo yetu moja kwa moja, lakini namshukuru Mwenyezi Mungu kwa uwepo wa mtandao huu pendwa wa jamii, unaosikiliza, kuchambua, kulinda, kuwasilisha, na kujali changamoto zote zinazowasilishwa hapa JF.
Mimi ni mdau na Mtanzania halisi. Kwa sasa tunapata shida kubwa sana upande wa huduma ya maji. Takribani wiki nzima sasa, maji yamekuwa tatizo kubwa ndani ya Jiji la Mwanza, hususan upande wa Isamilo.
Hali hii imekuwa tishio na ni hatari hasa kwa mama zetu, dada zetu, na watoto, maana inawalazimu kuamka usiku sana ili kuwahi foleni ya maji wasije wakakosa. Kwa wamiliki wa matenki, hali hii pia inaleta changamoto kubwa kwa wananchi.
Wito wangu ni kwa Serikali yetu kuangalia kwa makini suala hili, ili kuzuia changamoto kubwa zaidi za baadaye na kuhakikisha mahitaji ya maji kwa wote yanapatikana bila kero.
Ni wenu katika ujenzi wa taifa,
Kimwaga Campus
View attachment 3442375