Hehehe mnachekesha, limau nimekua natumia kila siku asubuhi kabla kula chochote kwa miaka kadhaa sasa hata kabla corona haijaja. Kawaida mimi kwa mafua huwa simezi vidonge na kunywa dawa, na sio mimi tu, huku Kenya tunafahamika sana kwenye kuzingatia sana masuala ya afya.
Nimewaambia mara kadhaa sasa kwamba tukiamua kuficha corona kama nyie inafichika tu, maana hadi sasa miezi yote hii hatujafa wengi, hiki kitu kwa namna moja au nyingine hakikuja na nia ya kutugaragaza Waafrika.
Tatizo ni kwamba Kenya hatuwezi kufuata namna ya mnavyofanya mambo huko ya kiujamaa, ambapo watu milioni 60 mnashikiliwa akili na kiongozi, hata wataalam wote hawana la kusema, sisi tumefundishwa kuhoji, huku rais hawezi akaamka mara moja na kufoka foka kwamba corona imeisha na kuchimba mikwara hataki kuiskia ikitajwa, na kuifanya corona iwe kama gonjwa la aibu kwamba mtu akiumwa inabidi kuwa siri ya ndani.
Wakenya tunaweza tukamvuruga rais Uhuru hadi atamani kuihama nchi, sisi tunataka tuhabarishwe hali kama ilivyo, takwimu zitolewe, tupimwe na tuendelee kuchukua tahadhari. Hili ni tatizo la kisayansi haliwezi kutoweka kwa matamko au hasira za rais.