Kwanza kabisa kitaalam na kisayansi hamna jipya mumelifanya maana ingekua mnapima na kuonyesha takwimu hazipandi, hapo ningeelewa kuna namna fulani mumejitibu, ila nakumbuka mwisho namba zenu zilipandisha usiku mmoja mkafikisha waathirika 509, rais akaibuka akafoka kwa ukali na kuanzia hiyo siku mkazima kila jitihada, mkaifanya corona kama aibu fulani, leo hii aibuke Mtanzania yeyote akubali hadharani anaumwa corona, atakemewa hadi kuzimu, mumefukia vichwa ardhini na kuamua kutesekea kila mmoja ndani kwa ndani.
Nawaambia na narudia tena, bahati yenu ni ile kwamba corona haiui Waafrika kwa wingi, hata kwa mataifa yetu ambayo hatujajichokea kama nyie tunaotoa taarifa kila siku, idadi za waliokufa kwa corona bado ndogo sana ukilinganisha na wanavyopukutika Ulaya, maana kwamba hata sisi tungeamua kuficha ingefichika tu, ni vile sisi na nyie tuna tofauti kubwa sana kimtazamo na kimaisha, kwenu huko imetosha rais kukemea hata janga la taifa kama corona na kila mtu akakunja mkia na kunyamaza kwa ndani, nakumbuka hata kwenye tetemeko la ardhi aliwafokea wahanga na kuwaambia hatowalipa kitu maana si yeye aliyeleta hilo janga, mkaufyata nyote, huo ndio mfumo wa kiujamaa, herd mentality.
Vifo vya corona bado vichache Afrika, na wanasiasa wanaumiza akili wakijaribu kujua nini sababu, hamna cha malimau na sijui pumba zipi hizo za kujifukiza, nakumbuka sijui alikua mbunge gani kwenu alikufa kwa corona, hotelini chumbani kwake kulikutwa vifaa vya kufukiza. Kuna kingine kinafanya Afrika tumepona kwa hili janga, imesemekana mataifa ambayo huwa na chanjo ya homa ya njano yanasalimika.
Mwenyewe hapa kuna kipindi niliumwa siku tatu, nikajua corona ndio imetia kambi, ila siku ya tatu nikaamka freshi na kudunda mtaani, na kawaida huwa nadungwa hiyo chanjo nikisafiri.
Hapa Kenya japo inatangazwa sana waathirika wapya, ila wanaopona ni wengi tu lakini inasubiriwa hadi wapimwe mara tatu ndio watangazwe kwamba wamepona na kuachiwa nje.
[/QUO
Tanzania hakuna corona wala siyo suala la kufukia vichwa chini! Huwezi kufukia vichwa chini mbele ya vifo kama vingekuwepo!! Hakuna Mzazi angekubali kupeleka MTOTO shule kama tunaona kwenye jamii wagonjwa ni wengi na vifo vinatokea. Kumbuka huwezi kuficha vifo!!
Kuhusu Kenya nyie ni Wa 7 barani afrika Kwa kuwa na wagonjwa wengi Wa corona. Siyo Kwa sababu mnapima maana hata Rwanda na Uganda wanapima sana. POLENI. Kinachosikitisha ni kwamba mpaka Sasa hamjajua tatizo ni nini.
Niwaambie tena tatizo LA kenya ni kuidhihaki Tanzania ilipoamua kumtegemea Mungu kwenye ugonjwa wa corona! Mungu akaamua kuonyesha tofauti kati ya anayemtegemea Mungu na yule anayemdhihaki yule anayemtegemea Mungu. Kenya itaendelea kuwa na corona mpaka hapo itakapouomba msamaha Tanzania kwa kutudhihaki na itakapomwomba Mungu msamaha pia. Vinginevyo hata mwakani shule zenu hazitafunguliwa!