chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Hili sio jambo la ajabu, sasa hivi kuna watu wanapisha SGR, kuna watu wanahamishwa kupisha upanuzi wa barabara, ujenzi wa sekondari, vyuo vikuu, stendi ya magufuli watu waliipisha, stendi ya nyamhongolo mwanza, ujenzi wa migodi.
Upanuzi wa viwanja vya ndege Mwanza na DSM, watu waliipisha, ujenzi wa makao makuu Dodoma, watu wamepisha na wanafidiwa.
Hata nyie ni sehemu ya Tanzania, mnahamishwa na mnafidiwa. Hapo kuna maslahi ya umma.
The Land Act.
The Village Land Act.
Land Acquision Act.
Zinasema ardhi ni Mali ya umma wa Tanzania, sio Mali ya wamasai. Mdhamini ni Rais, Umma ukihitaji ardhi, basi anayenyanganywa anafidiwa.
Umma una maslahi na utalii, unawaondoa, na unawafidia.
Wagogo wangekataa kutoa ardhi, ikulu ya chamwino ingejengwa? Mloganzila Ile hospitali ingejengwa? Bugando Hospitali ingejengwa? Hii miji mikubwa inapimwa na kupendez kwa sababu wakazi wa asili walikubali kuachia ardhi.
Kwa mujibu wa sheria sisi ni wapangaji katika ardhi, ndio maana tunalipa Kodi ya ardhi Kila mwaka. Mmiliki wa ardhi ni umma, Rais ni mdhamini. Umma umeamua kuwapa eneo jingine.
Hizi hifadhi mnazosikia maeneo mengine ya nchi, sisi pia tulihamishwa, hata Bunda na Busega, Kuna kipande kidogo sana ambacho watahamishwa ili kupisha njia ya wanyama kunywa maji ndani ya ziwa Victoria.
Haiwezekani, Ngorongoro iwe kwa ajili ya wanyama! Binadamu watoke humo