Wakazi wa Ngorongoro, tunawakumbusha tu kwamba hata sisi wa maeneo mengine ya Tanzania, kama Kuna maslahi ya umma, tulihamishwa

Wakazi wa Ngorongoro, tunawakumbusha tu kwamba hata sisi wa maeneo mengine ya Tanzania, kama Kuna maslahi ya umma, tulihamishwa

na hapa inapaswa kueleweka ni "kwa maslahi ya Taifa" fedha zinazopatikana kwenye hifadhi hiyo zinakwenda kusaidia wananchi wote na ni wajibu wa serikali kuilinda ili iendelee kusaidia kizazi hadi kizazi,hatuwezi kuruhusu ubinafsi wa wachache kuharibu rasilimali hii adhimu
kuhusu hoja mi sijali sana maana hata hoja yenyewe inaweza kuwa propaganda tu ,si tushazulumiwa sana na serikali lakin tulikubali maisha yaende. serikali kama ukuta tu wamasai wakubali yaishe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulishawahi kutembeza watalii au kutalii?!

Kaulize km kuna mzungu anaenda kuangalia wanyama ngorongoro bila kuomba kuwaona wamasai…

Hv hujawahi kukutana na matangazo ya kampuni za simu…wa kwanza alijitangaza kwamba yeye ni simba wa pili akajitangaza kuwa yeye ni Masai na mkuki..maana yake anauwa simba…

Tungejuaje km Masai anauwa simba km si tafiti za wazungu kuja na kukaa na wamasai nakujua maisha yao ya kila siku…maana kasuku km wewe hayo maarifa huna unajua kusubiria mikopo tuu upate mgao wako
Mkuu umepiga kwenye kidonda ndugu.
 
Kama Kuna mtu hajui kwa nini Ngorongoro inatakiwa Masai wahame huyo si mjinga tu ni mpumbavu kabisa.
Utalii na conservation ni vyanzo vya mapato. Kuzidi shughuli za binadamu ni kuua rasilimali hiyo. Lazima waondoke Masai sio lazma Kwa utalii na hata NCA Act imeelekeza natural activities. Waondoke haraka wanaobisha vunja miguu hivo hivo.
Kunzia 1970s wanabembelezwa wao nani.
Linda heritage at any cost
 
Hili sio jambo la ajabu, sasa hivi kuna watu wanapisha SGR, kuna watu wanahamishwa kupisha upanuzi wa barabara, ujenzi wa sekondari, vyuo vikuu, stendi ya magufuli watu waliipisha, stendi ya nyamhongolo mwanza, ujenzi wa migodi.

Upanuzi wa viwanja vya ndege Mwanza na DSM, watu waliipisha, ujenzi wa makao makuu Dodoma, watu wamepisha na wanafidiwa.

Hata nyie ni sehemu ya Tanzania, mnahamishwa na mnafidiwa. Hapo kuna maslahi ya umma.

The Land Act.
The Village Land Act.
Land Acquision Act.
Zinasema ardhi ni Mali ya umma wa Tanzania, sio Mali ya wamasai. Mdhamini ni Rais, Umma ukihitaji ardhi, basi anayenyanganywa anafidiwa.

Umma una maslahi na utalii, unawaondoa, na unawafidia.

Wagogo wangekataa kutoa ardhi, ikulu ya chamwino ingejengwa? Mloganzila Ile hospitali ingejengwa? Bugando Hospitali ingejengwa? Hii miji mikubwa inapimwa na kupendez kwa sababu wakazi wa asili walikubali kuachia ardhi.

Kwa mujibu wa sheria sisi ni wapangaji katika ardhi, ndio maana tunalipa Kodi ya ardhi Kila mwaka. Mmiliki wa ardhi ni umma, Rais ni mdhamini. Umma umeamua kuwapa eneo jingine.

Hizi hifadhi mnazosikia maeneo mengine ya nchi, sisi pia tulihamishwa, hata Bunda na Busega, Kuna kipande kidogo sana ambacho watahamishwa ili kupisha njia ya wanyama kunywa maji ndani ya ziwa Victoria.

Haiwezekani, Ngorongoro iwe kwa ajili ya wanyama! Binadamu watoke humoR
SeRikali imekuwa pole sana hii!!!?? Magufuli alivunja nyumba za watu kimara kama shetani
 
Wamekuwepo kwa miaka mingapi?

Sababu kuu za kuwahamisha ni zipi?

Toa sababu 5
Sababu zote tano za nini!? Sababu ni moja tu. Wamasai hamjaelimika na hamko tayari kuelimishwa
 
Ulishawahi kutembeza watalii au kutalii?!

Kaulize km kuna mzungu anaenda kuangalia wanyama ngorongoro bila kuomba kuwaona wamasai…

Hv hujawahi kukutana na matangazo ya kampuni za simu…wa kwanza alijitangaza kwamba yeye ni simba wa pili akajitangaza kuwa yeye ni Masai na mkuki..maana yake anauwa simba…

Tungejuaje km Masai anauwa simba km si tafiti za wazungu kuja na kukaa na wamasai nakujua maisha yao ya kila siku…maana kasuku km wewe hayo maarifa huna unajua kusubiria mikopo tuu upate mgao wako
Nonsense... upupu kwahiyo wakienda kuwaona ndio nini?? Mikumi kuna Wamasai? Serengeti kuna wamasai?

South Africa wana mbuga pale Klugger wana wana wamasai. Who are masai by the way??

Watatoka kilazima, hii nchi ni ya wote, hivyo pale serikali inapotaka kufanya jambo fulani utahamishwa tu.
 
Umetaja kuhamishwa kupisha miradi ya maendeleo.

Hawa hawahamishwi kupisha mradi wa maendeleo.

Bali wanafukuzwa kupisha waarabu wa Oman wakawinde na kubeba wanyama hai.

Hiyo ndio tofauti iliyopo.
Acha kupotosha watu. Wakati mwingine muwe mnaficha ujinga wenu.

Uwindaji na ukamataji wa wanyama ni biashara halali ambayo imekuwepo tangu kabla ya uhuru, baada ya uhuru na hadi sasa. Biashara hii hufanyika kwenye maeneo ya Game reserves, game controlled area, WMA, au maeneo ya wazi. Na haifanyiki kwenye maeneo ya hifadhi za taifa zilizo chini ya TANAPA na hifadhi ya Ngorongoro.

Loliondo ni Game controlled area ni kitalu cha uwindaji.

Idadi ya watu ndani ya hifadhi ya Ngorongoro imekuwa ikiongezeka kila mwaka. Aidha tabia za wanasai nazi zimeendekea kubadilika kama jamii nyingine. Wamasai wa mwanzo walikuwa hawalimi, sasa hivi wanalima; Wamasai wa zamani walikuwa wanaishi kwenye nyumba za miti na nyasi sasa hivi wanajenga nyumba za bati; Wamasai wa mwanzo walikuwa wanatembea kwa miguu sasa hivi wana pikipiki na magari. Wamasai wa mwanzo walikuwa hawali nyama pori sasa hivi wanakula...na mabadiliko mengine

Sasa unadhani kwa mabadiliko haya, na ongezeko la idadi...Ngorongoro itaweza kuhimili kwa muda gani kabla wanyama hawajatoweka?

Je unajua mchango wa Ngorongoro kwenye uchumi wa taifa ni kiasi gani? Ngorongoro ikutoweka uchumi utaathirija kiasi gani?
 
Nonsense... upupu kwahiyo wakienda kuwaona ndio nini?? Mikumi kuna Wamasai? Serengeti kuna wamasai?

South Africa wana mbuga pale Klugger wana wana wamasai. Who are masai by the way??

Watatoka kilazima, hii nchi ni ya wote, hivyo pale serikali inapotaka kufanya jambo fulani utahamishwa tu.

South Africa?!

Wewe una table mountain?!

Ndio maana Mikumi haitwi Ngorongoro

Everything has its own uniqueness…kumfukuza mmasai Ngorongoro ni sawa na kufukuza simba…

Hizo pesa mlizokula mzitapike…wamasai hawaondoki labda mkawaulie pale…umesikia wee msukule wa walamba asali
 
Sheria gani inasema hivyo? Uwekezaji nao ni maslahi ya umma we dogo.
Binadamu wanatakiwa kupisha kwa lazima mradi wa kijamii na sio wawekezaji.

Na ikiwa ni wawekezaji basi lazima pawe na mazungumzo hadi upatikane muafaka.
 
Hoja hii imeungwa mkono!
Serikali ya Tanzania ndiye mmiliki wa ardhi! Wengine hatuna uamuzi wa mwisho!

Na ukiamua imeamuliwa hata ziwekwe siasa za Aina gani watafanya jambo lao!
Kimara, sijui Kipawa, ilikuwa Lukobe huko Kilosa...Ihumwe...Songwe....Mvomero! Waathirika ni Sisi kwa ustawi wa jamii au hifadhi!
uma wa watanzania ndio wa miliki wa ardhi huku raisi akipewa mamlaka ya kusimamia ardhi na uma wa watanzania, kumbuka kusimamia ni tofauti na kumiliki. umma ndio unapaswa kuwa na kauli ya mwisho juu ardhi yao baada ya maridhianoo
ya pande zote mbili. Je wamasai wameridhia ardhi yao kunyakuliwakwa ajili huyo mnayesema muwekezaji?
je wamelipwa fidia ili kupisha uwekezaji?
huko Handeni waendako ni altenatively equal to masai land kwa ajiri ya ufugaji?
Je muwekezaji ni sawa na maslahi ya umaa? hata tofaitisha maslahi ya uma na uwekezaji wa uwindani, kwangu mimi uwindaji sio maslahi ya uma kwa sababu mnufaika mkuu ni muwekezaji.

Njia nzuri kuwa na mjadala mpana kati jamii ya masai na serikali kabla ya kutumia nguvu.

uwekezaji ni land grabing ama lan robbery, forced eviction.

warudi mezani kujadili ama huyo muwekezaji atafutiwe ardh inginne.
how can we displace the whole district in a name of public interest?

rejeeni mkazungumze myajenge upya naimani amani itatamalaki huko ngorongoro
 
Kama Kuna mtu hajui kwa nini Ngorongoro inatakiwa Masai wahame huyo si mjinga tu ni mpumbavu kabisa.
Utalii na conservation ni vyanzo vya mapato. Kuzidi shughuli za binadamu ni kuua rasilimali hiyo. Lazima waondoke Masai sio lazma Kwa utalii na hata NCA Act imeelekeza natural activities. Waondoke haraka wanaobisha vunja miguu hivo hivo.
Kunzia 1970s wanabembelezwa wao nani.
Linda heritage at any cost
Watu wamejazana ujinga. Muarabu ndiye anayepambaniwa ammilikishwe!

NGO zinajua zinaenda kufa kifo cha mende! Mahela waliyokuwa wanachukua kupitia mgongo wa mashuka na sime za wamaasai yanayeyuka na kupotea!
 
Back
Top Bottom