Wakazi wa Ngorongoro, tunawakumbusha tu kwamba hata sisi wa maeneo mengine ya Tanzania, kama Kuna maslahi ya umma, tulihamishwa

kuhusu hoja mi sijali sana maana hata hoja yenyewe inaweza kuwa propaganda tu ,si tushazulumiwa sana na serikali lakin tulikubali maisha yaende. serikali kama ukuta tu wamasai wakubali yaishe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umepiga kwenye kidonda ndugu.
 
Kama Kuna mtu hajui kwa nini Ngorongoro inatakiwa Masai wahame huyo si mjinga tu ni mpumbavu kabisa.
Utalii na conservation ni vyanzo vya mapato. Kuzidi shughuli za binadamu ni kuua rasilimali hiyo. Lazima waondoke Masai sio lazma Kwa utalii na hata NCA Act imeelekeza natural activities. Waondoke haraka wanaobisha vunja miguu hivo hivo.
Kunzia 1970s wanabembelezwa wao nani.
Linda heritage at any cost
 
SeRikali imekuwa pole sana hii!!!?? Magufuli alivunja nyumba za watu kimara kama shetani
 
Wamekuwepo kwa miaka mingapi?

Sababu kuu za kuwahamisha ni zipi?

Toa sababu 5
Sababu zote tano za nini!? Sababu ni moja tu. Wamasai hamjaelimika na hamko tayari kuelimishwa
 
Nonsense... upupu kwahiyo wakienda kuwaona ndio nini?? Mikumi kuna Wamasai? Serengeti kuna wamasai?

South Africa wana mbuga pale Klugger wana wana wamasai. Who are masai by the way??

Watatoka kilazima, hii nchi ni ya wote, hivyo pale serikali inapotaka kufanya jambo fulani utahamishwa tu.
 
Umetaja kuhamishwa kupisha miradi ya maendeleo.

Hawa hawahamishwi kupisha mradi wa maendeleo.

Bali wanafukuzwa kupisha waarabu wa Oman wakawinde na kubeba wanyama hai.

Hiyo ndio tofauti iliyopo.
Acha kupotosha watu. Wakati mwingine muwe mnaficha ujinga wenu.

Uwindaji na ukamataji wa wanyama ni biashara halali ambayo imekuwepo tangu kabla ya uhuru, baada ya uhuru na hadi sasa. Biashara hii hufanyika kwenye maeneo ya Game reserves, game controlled area, WMA, au maeneo ya wazi. Na haifanyiki kwenye maeneo ya hifadhi za taifa zilizo chini ya TANAPA na hifadhi ya Ngorongoro.

Loliondo ni Game controlled area ni kitalu cha uwindaji.

Idadi ya watu ndani ya hifadhi ya Ngorongoro imekuwa ikiongezeka kila mwaka. Aidha tabia za wanasai nazi zimeendekea kubadilika kama jamii nyingine. Wamasai wa mwanzo walikuwa hawalimi, sasa hivi wanalima; Wamasai wa zamani walikuwa wanaishi kwenye nyumba za miti na nyasi sasa hivi wanajenga nyumba za bati; Wamasai wa mwanzo walikuwa wanatembea kwa miguu sasa hivi wana pikipiki na magari. Wamasai wa mwanzo walikuwa hawali nyama pori sasa hivi wanakula...na mabadiliko mengine

Sasa unadhani kwa mabadiliko haya, na ongezeko la idadi...Ngorongoro itaweza kuhimili kwa muda gani kabla wanyama hawajatoweka?

Je unajua mchango wa Ngorongoro kwenye uchumi wa taifa ni kiasi gani? Ngorongoro ikutoweka uchumi utaathirija kiasi gani?
 

South Africa?!

Wewe una table mountain?!

Ndio maana Mikumi haitwi Ngorongoro

Everything has its own uniqueness…kumfukuza mmasai Ngorongoro ni sawa na kufukuza simba…

Hizo pesa mlizokula mzitapike…wamasai hawaondoki labda mkawaulie pale…umesikia wee msukule wa walamba asali
 
Sheria gani inasema hivyo? Uwekezaji nao ni maslahi ya umma we dogo.
Binadamu wanatakiwa kupisha kwa lazima mradi wa kijamii na sio wawekezaji.

Na ikiwa ni wawekezaji basi lazima pawe na mazungumzo hadi upatikane muafaka.
 
uma wa watanzania ndio wa miliki wa ardhi huku raisi akipewa mamlaka ya kusimamia ardhi na uma wa watanzania, kumbuka kusimamia ni tofauti na kumiliki. umma ndio unapaswa kuwa na kauli ya mwisho juu ardhi yao baada ya maridhianoo
ya pande zote mbili. Je wamasai wameridhia ardhi yao kunyakuliwakwa ajili huyo mnayesema muwekezaji?
je wamelipwa fidia ili kupisha uwekezaji?
huko Handeni waendako ni altenatively equal to masai land kwa ajiri ya ufugaji?
Je muwekezaji ni sawa na maslahi ya umaa? hata tofaitisha maslahi ya uma na uwekezaji wa uwindani, kwangu mimi uwindaji sio maslahi ya uma kwa sababu mnufaika mkuu ni muwekezaji.

Njia nzuri kuwa na mjadala mpana kati jamii ya masai na serikali kabla ya kutumia nguvu.

uwekezaji ni land grabing ama lan robbery, forced eviction.

warudi mezani kujadili ama huyo muwekezaji atafutiwe ardh inginne.
how can we displace the whole district in a name of public interest?

rejeeni mkazungumze myajenge upya naimani amani itatamalaki huko ngorongoro
 
Watu wamejazana ujinga. Muarabu ndiye anayepambaniwa ammilikishwe!

NGO zinajua zinaenda kufa kifo cha mende! Mahela waliyokuwa wanachukua kupitia mgongo wa mashuka na sime za wamaasai yanayeyuka na kupotea!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…