KERO Wakazi wa Ubungo–Msewe bado tunanunua ndoo ya maji Sh 1,300 hadi 1,500

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakazi wa Ubungo–Msewe, Dar es Salaam tuna changamoto kubwa ya maji kwa sasa kuanzia mwezi wa 12 mwaka 2025.

Kwa sasa maji ya mgao yanaweza toka baada ya wiki 3 au mwezi nayo huwa yanatoka mara moja tu kwa huo muda kuanzia saa saba usiku mpaka saa 10 alfajiri.

Hali imekuwa ngumu kiasi kwamba tunalazimika kununua maji dumu moja la maji kuanzia TSh 1,300–1,500 mpaka maji yafikishwe unapoishi, jambo ambalo ni gharama kubwa kwa wananchi, hasa kwa familia zinazohitaji maji kila siku.

Tunaomba utusaidie kuifikisha sauti hii kwa mamlaka husika, ili tupate majibu ya kweli kuhusu tatizo hili na ikiwezekana tupatiwe suluhisho la kudumu, si kuendelea kutegemea kununua maji kwa gharama kubwa.

Tunaamini ukitupazia sauti yako, ujumbe huu utafika kwa wahusika na hatua zitachukuliwa kwa ajili ya wakazi wa Ubungo – Msewe na maeneo yanayozunguka.
 
Duh nimewahi kukaa hapo enzi za chuo karibu na pori la mfuga paka! Maji mitaa hiyo ni mtihani sio poa.
 
Fursa hyo kijana tafuta gutha l kukodi nunua boza/tank/pipa/madumu jaza maji ingia msewe upige pesa
 
Nimekulia mitaa ya hapo Kibo aisee shida ya maji ambayo ipo mitaa hiyo ya Kibo na Msewe ni ya miaka na miaka
 
Wakazi wa Ubungo–Msewe, Dar es Salaam tuna changamoto kubwa ya maji kwa sasa kuanzia mwezi wa 12 mwaka 2025.

Kwa sasa maji ya mgao yanaweza toka baada ya wiki 3 au mwezi nayo huwa yanatoka mara moja tu kwa huo muda kuanzia saa saba usiku mpaka saa 10 alfajiri.

Hali imekuwa ngumu kiasi kwamba tunalazimika kununua maji dumu moja la maji kuanzia TSh 1,300–1,500 mpaka maji yafikishwe unapoishi, jambo ambalo ni gharama kubwa kwa wananchi, hasa kwa familia zinazohitaji maji kila siku.

Tunaomba utusaidie kuifikisha sauti hii kwa mamlaka husika, ili tupate majibu ya kweli kuhusu tatizo hili na ikiwezekana tupatiwe suluhisho la kudumu, si kuendelea kutegemea kununua maji kwa gharama kubwa.

Tunaamini ukitupazia sauti yako, ujumbe huu utafika kwa wahusika na hatua zitachukuliwa kwa ajili ya wakazi wa Ubungo – Msewe na maeneo yanayozunguka.
Nyie mmekimbilia kupanga huko ili mrahisishe kwenda chuo ndo kimewatokea cha kuwatokea poleni sana.
Hakia kimara mbezi maji ndoo sh.200
 
Hapa ndipo ilipotofauti ya masikini na tajiri. Sisi tunaona changamoto kwa kila fursa ila tajiri huona fursa kwa kila changamoto.
 
Wakazi wa Ubungo–Msewe, Dar es Salaam tuna changamoto kubwa ya maji kwa sasa kuanzia mwezi wa 12 mwaka 2025.

Kwa sasa maji ya mgao yanaweza toka baada ya wiki 3 au mwezi nayo huwa yanatoka mara moja tu kwa huo muda kuanzia saa saba usiku mpaka saa 10 alfajiri.

Hali imekuwa ngumu kiasi kwamba tunalazimika kununua maji dumu moja la maji kuanzia TSh 1,300–1,500 mpaka maji yafikishwe unapoishi, jambo ambalo ni gharama kubwa kwa wananchi, hasa kwa familia zinazohitaji maji kila siku.

Tunaomba utusaidie kuifikisha sauti hii kwa mamlaka husika, ili tupate majibu ya kweli kuhusu tatizo hili na ikiwezekana tupatiwe suluhisho la kudumu, si kuendelea kutegemea kununua maji kwa gharama kubwa.

Tunaamini ukitupazia sauti yako, ujumbe huu utafika kwa wahusika na hatua zitachukuliwa kwa ajili ya wakazi wa Ubungo – Msewe na maeneo yanayozunguka.
Hiyo ni sawa kwakuwa mnapanga na kodi ni bei rahisi, sisi huku Masaki maji ni kama bure ila kodi ni milioni 3 kwa mwezi.
 
Poleni sana huku mvuti Dondwe maji yanatiririka bombani bila kukatika!...
 
Wakazi wa Ubungo–Msewe, Dar es Salaam tuna changamoto kubwa ya maji kwa sasa kuanzia mwezi wa 12 mwaka 2025.

Kwa sasa maji ya mgao yanaweza toka baada ya wiki 3 au mwezi nayo huwa yanatoka mara moja tu kwa huo muda kuanzia saa saba usiku mpaka saa 10 alfajiri.

Hali imekuwa ngumu kiasi kwamba tunalazimika kununua maji dumu moja la maji kuanzia TSh 1,300–1,500 mpaka maji yafikishwe unapoishi, jambo ambalo ni gharama kubwa kwa wananchi, hasa kwa familia zinazohitaji maji kila siku.

Tunaomba utusaidie kuifikisha sauti hii kwa mamlaka husika, ili tupate majibu ya kweli kuhusu tatizo hili na ikiwezekana tupatiwe suluhisho la kudumu, si kuendelea kutegemea kununua maji kwa gharama kubwa.

Tunaamini ukitupazia sauti yako, ujumbe huu utafika kwa wahusika na hatua zitachukuliwa kwa ajili ya wakazi wa Ubungo – Msewe na maeneo yanayozunguka.
Inasikitisha sana.

Mbunge wenu ni Mzee wa Mipango na Dira halafu Mpango wa kutatua Kero za Maji kashindwa.
 
Back
Top Bottom