A
Poleni sana, mimi nikajua kinyerezi umeme haukatiki maana nampango wa kuhamia huko.Mimi ni mkazi wa Ulongoni A karibu na Bar ya Magogoni, Mtaa unaitwa kwa Makamba Jijini Dar es Salam hapa Ilala upande Kinyerezi, kero yangu ni umeme kukatika katika kila mara ifikapo saa moja jioni, yaani umeme unaweza kukatika hata mara 50 kwenye saa moja.
Tumeshawasilisha kero hii Tanesco kwa kuwapigia mara nyingi sana ila hawajawahi kutatua tatizo hili.
Wanasema watakuja kufunga Transfoma kila siku na tangu nimehamia mtaa huu ni mwaka wa nne sasa.
Tunaiomba mamlaka husika ifuatilie na kutatua tatizo hili haraka iwezekanavyo kwani wananchi tunaathirika kwa kiwango kikubwa. Tunaamini huduma bora na ya uhakika ya umeme ni haki ya kila mwananchi.
Habari, ndugu mteja.Mimi ni mkazi wa Ulongoni A karibu na Bar ya Magogoni, Mtaa unaitwa kwa Makamba Jijini Dar es Salam hapa Ilala upande Kinyerezi, kero yangu ni umeme kukatika katika kila mara ifikapo saa moja jioni, yaani umeme unaweza kukatika hata mara 50 kwenye saa moja.