KERO Wakazi wa Wikichi, Njombe, tunalalamikia milipuko ya baruti karibu na makazi

KERO Wakazi wa Wikichi, Njombe, tunalalamikia milipuko ya baruti karibu na makazi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari JF,

Kuna kero kubwa katika Mtaa wa Wikichi, Halmashauri ya Mji wa Njombe, inayosababishwa na wachimbaji na wapasuaji wa miamba ya mawe kwa ajili ya ujenzi.

Wachimbaji hao wanatumia vilipuzi kama baruti vinavyosababisha milipuko mikubwa na mitetemo inayofanana na milipuko ya mabomu. Kinachotia wasiwasi zaidi ni kwamba shughuli hizo zinafanyika karibu na makazi ya watu, takribani mita 200 kutoka kwenye nyumba za wakazi.

Milipuko hiyo inasikika kwa nguvu kiasi cha kutikisa nyumba na kusababisha hofu miongoni mwa wakazi. Watoto hukimbia kwa taharuki kila milipuko inapotokea, huku baadhi ya wakazi wakilalamikia maumivu ya masikio kutokana na sauti hizo kali.

Jambo la kusikitisha ni kwamba shughuli hizo zinaonekana kufanyika bila tahadhari za kutosha kuzingatia afya na usalama wa watu wanaoishi jirani na machimbo hayo.

Tunaomba Serikali na mamlaka husika zifike eneo hilo kuchunguza shughuli hizo na kuhakikisha kuwa vilipuzi vinatumika kwa kuzingatia sheria, taratibu na viwango vya usalama vinavyotakiwa.

Soma Pia: Milipuko ya mwekezaji kupasua mawe Mtaa wa Makutano – Sumbawanga unatukwaza Wakazi wa hapo

Je, ni sahihi shughuli za ulipuaji wa miamba kuendelea karibu na makazi ya watu bila hatua madhubuti za kulinda usalama wao?
Tunaomba hatua zichukuliwe kabla madhara makubwa hayajatokea.
 
Back
Top Bottom