Wakazi/wenyeji wa Iringa naombeni muongozo wenu

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2020
Posts
9,016
Reaction score
24,650
Kwa sasa makazi yangu ni Iringa mjini hapa Kihesa. Shughuli niliyokua nafanya kwa kiasi kikubwa inategemea jua kuwaka mchana na sasa ni kipindi cha mvua ivyo kazi haifanyiki

Kwa wajanja janja wa huu mkoa nina akiba ya 500K naweza kufanya mishe gani kwa kipindi cha mvua ila tu isiwe kilimo
 
Fanya kwa utafiti tembelea mitaa Kama semtema, tumaini, stendi y dodoma hapo, mjini na sehem zngne utapata idea tu pia Kuna sehem mpk Sasa hazina mvua hvyo zitembelee mfno pagawa, migori na nk.

Sema now sipo Iringa but karibu Iringa mzee Karibu TRM.
 
1. Njoo Dar karume chagua viatu vizuri vya wadada zungusha chuo Cha Tumaini, Mkwawa na Iringa University.

2. Njoo Dar Ilala tafuta skin jeans nzuri, blauzi na sweta za kistaduu kauze kwenye vyuo tajwa hapo au mwaga pale mashinetatu.

3. Njoo Dar tafuta machimbo ya vile vitambaa ambavyo tandika wanauza mita 2500, kata aina tofauti tofauti, kamwage mashine tatu uza (hii biashara Iringa haipo kabisa Hadi uende madukani uhindini napo ni Bei kubwa)

4. Ukishindwa kabisa tafuta mama ntilie kadhaa walio na mtaji mdogo waongeze mtaji wa elfu hamsini tu waambie muwe mnashare wewe faida Yako ni 1500 Kwa siku kwenye elfu 50

Karibu Iringa mkuu, Ulanzi mtogwa ukiwa mwingi nitumie nienzi mkoa wangu.
 
Idea nzuri Sana
 
Kuna vyuo viingi vikubwa vimerundikana katikati ya jiji ni wewe na akili yako tu!
 
Back
Top Bottom