Lizzy haki yao kama ni kuachika na wajibu wao ni upi?..........................
hakuna haki bila ya wajibu, you know that.......
Tunapozungumza HAKI NA WAJIBU tuliangalie suala hili katika hali ya mlalo (horizontally) na sio ya wima (vertically) kwa maana ya kuwa mmoja anatakiwa apewe haki mwengie hataki kutimiza wajibu.
Binafsi sipendelei sana NDoa za Mkeka, japo mimi Ni Muislamu, lakini watoto wa siku hizi wamezidi kufanya mambo yasiyofaa, mzazi anaona labda akimfanya vile huenda Binti atatulia, na pia ni katika kuondoa DHIMMA ya Mzazi kuepusha Zinaa. mkumbuke kuwa Zanzibar ni nchi ambayo wakaazi wake ni 95% waislamu na ni wazazi ambao wanaishi kwa misingi ya Dini yao! hivo wanaepusha Zinaa. tatizo kubwa linakuja kwa watoto wa kiume nia yao nadhani ni kufanya Zinaa akimshamchezea Binti akimbie. sasa Mzazi hakubali hili anaona bora amuozeshe! anaepuka Zinaa na pia huenda binti akatulia.
Kwa kiasi kikubwa ndoa za mkeka ni sababu ya talaka. Bila ya kufanya utafiti, nahisi asilimia kubwa ya ndoa za mkeka hazidumu (mawazo binafsi).
kule unakuta mtu ana wake 3,kazi anayofanya ni kuvua samaki-at local and primitive way,hawezi kukidhi mahitaji ya familia,na anatumia sheria za dini kuforce submission kutoka kwa wake zake-regardless huyo mr yupo right or wrong-so kwa wanawake wasiopenda kuonewa,lazima wakimbie kwa mtu kama huyu wakajilimie mwani
Uko sahihi Bro kwa kuzingatia hayo nilyoweka red isipokuwa hilo la mwisho "wanawake wasiopenda kuonewa" ambalo nahisi HAKUNA binadamu anayependa kuonewa. Lakini si suala la kipato kidogo tu linalovunja ndoa bali suala la unyanyasaji vileviel. Wengine hutumia kipato chao kama silaha ya kunyanyasa wake zao; na bado kuna wengine pamoja na kipato kikubwa, hawatimizi wajibu wao katika ndoa - hawaheshimu ndoa zao kwa uasherati na hawatoi
dozi inayostahiki. Usishangae kuona ke wa tajiri anatembea na mtunza bustani.
Yaani kweli wanawake wa Zenj hawana shukrani !!!! Huko si ndio nasikia kuwa mwanamke kazi yake kukaa ndani tu na kujichora na hina; mwanaume aleta kila kitu ikiwa ni pamoja na kwanda marikiti ?
Haya mambo ya kusikia haya.....!!!
wake wakidai walimwe talaka tatu na waume zao baada ya kuchoshwa na vitendo vya unyanywasaji, kutelekezwa na kudhalilishwa na waume zao................katika makala hii ya habari leo isomekayo kama.............Utoaji talaka wakithiri Zanzibar inathibitisha ya kuwa ndoa zimeparanganyika sana kule visiwani kama huku bara kutokana na waume kushindwa kubeba majukumu yao........................hatujui kwa kiasi gani na hao wake wameshindwa kubeba majukumu yao hususani la utii kwa waumme zao hata kusababisha kujikuta wanapata mateso makubwa kwa kisa "wameolewa"....................
Ikiwa taarifa hii umeiwasilisha kama ilivyoandikwa, nahisi inajitosheleza wala haihitaji kutafuta mchawi wa pili. Taarifa inasema na kusisitiza..."wake wanadai talaka
baada ya kuchoshwa na vitendo vya unyanywasaji, kutelekezwa na kudhalilishwa na waume zao.....ndoa zimeparanganyika sana kule visiwani kutokana na waume kushindwa kubeba majukumu yao....."
Sasa Ruta Mkuu, ikiwa mume ni mnyanyasaji, mtelekezaji, mdhalilishaji, anayeshindwa kubeba majukumu yake (kwa mujibu wa taarifa ya kadhi na kusisitizwa na maelezo yako), bado unahisi kuna haja ya kudai mke atakeleze majukumu yake? Tuseme hayo matendo ya mwanamme yanatokana na mwanamke kutotimiza wajibu wake?
Kama nlivyodokeza kule juu kuhusu haki na wajibu, hivi vitu vinakwenda sambamba kwa wakati mmoja, mwenye wajibu atekeleze kabla ya kudai haki, na kwa kadhia hii tunaona kuwa mwanamme ndiye kwa kupitia matendo kadhaa anakiuka wajibu wake. Bahati mbaya suala la ndoa linaangukia sana kwenye dini, utamaduni na mfumo ambapo yote matatu kwa bahati mbaya mwanamke/mke anakuwa "raia wa pili", wa kwanza akiwa mwanamme/mume.