Wake wa Marais wetu na Mambo yao

nchi inawanyonyaji wa kila aina hii !! khaaa
kumkopesha mwalimu kwa riba ya asilimia 200 ni kumnyanyasa hasa
shame on them
 
Tusaidie mzee... huo utafiti ulifanywa lini, na nani, na wapi, na unahusiana vipi na walimu wa jimbo la Zambi?

MWANAKIJIJI MSAIDIE ZAMBI AUONE UKWELI HUO MAPEMA KABLA HAJAINGIA MATATANI.

NIKUPE TU KITU KIDOGO CHA KUJIULIZA" Ni kweli nchi ina nyang'au wengi ila inatia shaka pale Mzee Kaduma anapobarikiwa kuwa naye ni mnyonyaji wa 200% tena kwa waalimu wa vijijini, maana hata FINCA na PRIDE hawajafikia RIBA hiyo mpya yenye rekodi duniani.

Nimekupa hizo ili usinihangaike nami bali tumia hekima ku conclude yaliyojiri.
 
nchi inawanyonyaji wa kila aina hii !! khaaa
kumkopesha mwalimu kwa riba ya asilimia 200 ni kumnyanyasa hasa
shame on them

Na hao walimu wanaokopeshwa kwa riba ya 200 haziwatoshi.hata wao shame on them
 
Nafikiri tunahitaji more info za pande mbilikatika hili swala!!
 
Sasa hii nao kali, tusubiri upande wa pili tujue moja
 
riba ya asilimia 200 haitokuwa jambo la kwanza la rekodi duniani kufanyika tanzania
 

I regret you are "a small mind". Least IQ in the world! (politely speaking: you must develope your IQ, it may be domant!!
 

Best business to do in the world! Jamani kwani hao walimu wanalazimishwa kukopa? Anyway; many companies (financial houses) will opt for such business! 1 million for 3 million; the best business!
 
Tusaidie mzee... huo utafiti ulifanywa lini, na nani, na wapi, na unahusiana vipi na walimu wa jimbo la Zambi?

Huyu mbunge inabidi ajieleze zaidi, convincingly with evidence.Tunapenda kumkoma Nyani lakini tunataka vitu solid.
 
ehhh kaazi kweli kweli!
kweli tanzania akili mukichwa unaweza tengenesa mapesa kwa mukichwa yako tu!
kama ni kweli hii ni dhulma!
 
Best business to do in the world! Jamani kwani hao walimu wanalazimishwa kukopa? Anyway; many companies (financial houses) will opt for such business! 1 million for 3 million; the best business!

Sishangai sana pia kwamba riba ni 200%, unajua bongo hawa wafanya biashara ya pesa wanatuumiza sana walala hoi! Wanaujanja wa kueleza figure zao wakificha makato halisi unayo garamia mkopaji ama mteja.

Nilishangaa pia jamaa yangu alichukua mkopo CRDB akaambiwa riba ni 15%, so akachukua 12mil kwa five yrs, ila alipo kuja piga mahesabu alijikuta analipa over 17 mil. ambayo ni 47% na si 15%, yaani kuna hesabu fulani zinapigwa hapo, huenda hata huyo mama wanachukua kwa riba ya 60% wakija changanua labda kwa miaka 3-5 wanajikuta wanalipa hiyo 200%

Amabacho sielewi, hivi BOT I mean mfumo wa banki nchini hauwezi kuwa regulated kiasi kwamba riba zikashuka kama nchi za wenzetu?
 
Ila mzee MKJJ iwa hueleweki eti huyu mama ni safi??
Mhh shemeji yako nini?Mbona mkuu hatukuelewi msimamo wako?Watu walisha shusha DATA kibao kuhusu huyu mama kuwa ni mchafu hawezi kutakata kwa sabuni yeyote ile.Na ndie aliyemwingiza majaribuni mzee Ben lakini ndo hivyo tena mnasema msafi au ndo kampeni ya kumsafisha nini huyu mama.Ngoja tusubili kesho nini kitaendelea.
 
HTML:
BayPort Financial Services.
wataalamu wa makampuni hebu tupeni uhalali wa hii kampuni je haikusajiliwa siku ya sikukuu? na inalipa kodi? kinanani major shareholders? kuna harufu ya fitna hapa.

Mimi si mtaalam wa makampuni...lakini nime gugo na nikapata info hii hapa chini.

 

Kwenye mambo ya mikopo kwanza inabidi mkopaji ajihakikishe aina ya interest anayotozwa, kwani kuna interest ya kawaida ambayo ambayo riba haitozwi riba, lakini kuna riba inayotozwa riba (Compound interest) ambayo nadhani ndiyo mabenk na makampuni kama Bayport wanatumia. Na mara nyingi riba hiyo inatozwa kwa mwezi na interest nayo inatozwa riba. Kwa hiyo inabidi unapokopa ukokotoe mahesabu ujue mwisho wa siku utalipa kiasi gani. yaani, Mkopo + cummulative interest.

Wataalamu wa mambo ya benki humu JF wanaweza kutusaidia hapa nini huwa kinafanyika katika kukokotoa hizo riba.

Rwabugiri, kama rafiki yako alikopa 12million na akalipa zaidi ya 17million kwa muda wa miaka nitano, kimahesabu ni sawa kabisa alitakiwa alipe 21,000,000 kwa hiyo gharama ya mkopo wote kwa miaka mitano ni 9,000,000. Hesabu yake ni rahisi tu (gharama ya riba = (Kiasi cha mkopo x riba (15%) x muda wa mkopo (5 years))/100).

Mkopo + Gharama ya mkopo = 21,000,000. Hivyo hakulipa 47% bali 15%. Tatizo la mkopo ni kwamba ukikopa pesa nyingi kwa muda mrefu gharama ya mkopo inakuwa kubwa. Kama angekopa hizo pesa na kulipa ndani ya mwaka mmoja angerudisha 13, 800,000/= (Mkopo + Interest). Hapo utaona gharama ya mkopo kwa mwaka mmoja ni 1,800,000/=
 
Kauli ya Zambi, itaibuka kesho kwenye magazeti kwa kuwa wanayoyasema bungeni yanakuwa na kinga.

Sio kweli yanayosemwa bungeni yanakuwa na kinga. Kuna qualifications.

Ndio maana Waziri Marmo alimtisha Slaa kwamba anavunja sheria kutoa siri za Serikali za Meremeta.

Ndio maana kila siku Wabunge wanamuuiliza Sitta, ninalindwa nikisema hili na lile...kana kwamba Sitta ni jaji au wakili wao.

For the record.
 
..nani aliwashikia bunduki hao Waalimu ili wakakope kwa Mama Mkapa?

..nilitegemea hiyo benki inayotoza riba 200% ingekufa mara moja kwa kukosa wateja.
 
..nani aliwashikia bunduki hao Waalimu ili wakakope kwa Mama Mkapa?

..nilitegemea hiyo benki inayotoza riba 200% ingekufa mara moja kwa kukosa wateja.

Ndio maana hata mimi nasema shame on this teachers hawana hata IQ ndogo ya kufikiria hiyo rate wanayotoswa au huyu aliyepost hii kitu atupe maelezo ya zaidi ni kwa rate gani wanatoswa kwa kulingana na kiasi la sivyo na sisi tutakuwa kichwa cha mwendawazimu kujadili habari nusu ambazo hazina kichwa wala miguu.
 

Kuhani, yanayosemwa Bungeni yanakuwa na kinga kwa maana ya kwamba anayosema Mbunge huwezi kumfikisha mahakamani kwayo. Hii hata hivyo ni tofauti na kusema kuwa Mbunge amelipotosha Bunge n.k kwani Bunge linauwezi wa kumchukulia hatua na si mahakama. Hii ni kesi ambayo imelindwa sana katika parliamentary democracy.

Wabunge wanaweza kumsema mtu yeyote, na kuibua lolote pasipo hofu ya kushtakiwa. Hofu pekee ni ya kufukuzwa Bungeni, kukosa kura, kusimamishwa n.k lakini siyo kushtakiwa mahakamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…