Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
WATUMISHI WA MUNGU ACHENI HUU UPUMBAVU NA UKENGEUFU!🔥🔥🔥
Mitume,manabii,wachungaji hili linawahusu.Mnakosea sana kuwatumia wanawake vibaya kinyume na maandiko.
Nabii Musa pamoja na miujiza yote aliyojaaliwa,alikuwa na mtumishi mmoja tu tena kijana wakiume,yaani Joshua.Nabii Eliya naye alihudumiwa na Elisha tu na sio wanawake kibao,tena wake za watu.Yesu Kristo alihudumiwa na wanawake kwa kupewa tu sadaka na mahitaji yake.Hii tabia yenu ya kuwapangia wake za watu kuwafanyia kazi za wake zenu mmeipata kwenye Biblia gani? Majukumu ya wake zenu kwa nini yafanywe na wasichana na wanawake wa kanisani?
Hii sio sawa watumishi wa Mungu kutumikiwa na wake za watu na wasichana kwenye ofisi,wala nyumbani kwa kuwapangia zamu;na kuwadanganya eti ndio kuteka baraka za Mungu. Ni upumbavu na ukengeufu tu wewe mhubiri kufuliwa nguo zako mpaka za ndani,na kusafishiwa nyumba yako na wake za watu na wasichana wa kanisani,wakati una mke wako na watoto. Hii ndio imewafanya wanaume wengi wakatae wokovu kwani hawana imani na tabia zenu.Hivi kazi za wake zenu ni zipi hasa?! Hebu waheshimuni wake zenu na acheni kuwatumia vibaya wanawake mnao waongoza.
Kanisa sio mali yenu bali ni la Yesu Kristo,aliyeenda msalabani.Ole wenu ninyi mnao litaabisha kanisa la Yesu Kristo kwa upumbavu na ukengeufu huu na kuwakosesha wengi.Upumbavu huu umesababisha ndoa nyingi kutokuwa na amani na umewafanya watu wengine waone wokovu ni majanga.Upako wako usiwe sababu ya kuwatumia watu vibaya na kulifanya jina la Yesu Kristo litukanwe.Halafu na ninyi wanawake acheni tabia mbaya ya kujipendekeza kwa watumishi wa Mungu;kwa kuingilia majukumu ya wake zao.Hiyo siyo baraka ya Mungu.Toeni sadaka na huduma zisizo na ukakasi wala maswali yenye utata kwa kanisa na jamii.Nawaonya kwani nami ninaye Roho Mtakatifu.
Jiunge kwa mafundisho ya Neno la Mungu kila siku kwa njia ya saut