Wakenya 35 wakamatwa Tarime na kuwekwa chini ya Karantini

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617
Watu 35 wanaodaiwa kuingia nchini kinyemela wakitokea nchini Kenya wamewekwa karantini kwa siku kumi na nne huku serikali wilayani Tarime mkoani Mara ikifunga maegesho yote ya waendesha bodaboda yaliyo kwenye mipaka ya Tanzania na Kenya kutokana na madereva hao kudaiwa kutumika kuwavusha raia wakigeni kuingia nchini.

====

Kipindi hiki ndicho kinatoa picha halisi yenye kuonyesha kati ya Tanzania na Kenya ni nani anayemtegemea na kumuhitaji mwengine.

Kule Horohoro, wakenya 24 walikamatwa na kurudishwa Kenya na pikipiki 10 za Kenya kutaifishwa, kuna wale waliotoroka baada ya Jirani kufariki kwa kuogopa Corona, Leo hili kundi la wakenya 35 limekatwa, wote hawa wanatumia njia za panya kuingia Tanzania, hii inatoa picha gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wengine wamedakiwa Geita yaani wameleta tafrani wako Karantini wote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njaa kali.
Yani Pale Kenya maisha yapo nairobi tu.
Ukitoka ukienda sehemu zingine ni njaa tupu.
Tanzania inabidi ifunge mpaka wake na Kenya.

Au kama vipi wabadilishe mipaka. Kuna vipande vya kenya tuvichukue , Kwanza jeshi la Kenya ni utopolo mtupu
 
Nina wasi waai sana mbona hizi kamata kamata zinazohusishwa na korona zimeanza baada ya statement za makonda? Kwamba wanaokaa ndani wanaiita corona inavyoonesha kutakua pia na ukamataji wawatu mbali mbali kwa kisingizio kua wanazusha taharuki lengo ni kuwatisha wananchi wasiseme ukweli kuhusu corona..na kutakua na katazo maalum watu wasizungumzie corona kama vile walivyo wahi kataza watu wasiseme vyuma vimekaza wakati mtaani hali ni tete.
 
Kweli Mkuu.
 
Ufipa hadi hii mnapinga!
 
Kweli Mkuu.
Tuliwaambia wakenya mnaitegemea sana Tanzania mlikua mbabisha, sasa unaona ukweli unavyojitokeza?. Hapo ni kwamba bado vyakula vinaruhusiwa kuingia Kenya toka Tanzania na Uganda, tukiamua kufunga mpaka kabisa, wakenya watakaokamatwa kujaribu kukimbilia Tanzania kwa siku, watazidi milioni moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MK254 huonekani nyuzi kama hizi,umekomaa na 5G za Gwajima tu.... Em Pitia hapa kwanza.

Uzi huwa naangalia kwanza nani kauleta kabla nifungue kuusoma, maana nyingi ukiangalia huwa hazina source wala nini, mtu kakurupuka tu na kuandika andika.
Sema kama ni kweli ningependa uhamiaji wa nchi yetu wajifunze kitu kutoka kwa wenzao wa Tanzania, maana huku kuna mpaka Watanzania wanaopatikana kuingia na Corona kabisa, Watanzania wengi waningia tu hivi hivi wanatushkiza huku Kenya kati, hujui mtu alitumia mbinu gani mpaka anafika kote huku.
Natumai serikali ilijifunza kitu baada ya taarifa za yule Mtanzania aliyepatikana amekuja na Corona, labda wataanza kulinda ipasavyo.
 
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Watanzania hawatumii njia za Panya, wanapita na kufuata sheria zote za mipaka ya hizi nchi mbili.

Mambo kama haya yakudhibiti watu kuingia na kutoka ndio yanayosababisha Kenya maambukizi kuongezeka kwa kasi sana, na maambukizi kuwa machache huku Tanzania.

Badala ya kuweka mkazo katika kuzuia maambukizi kuingia nchini mwenu, ninyi mnasubiri wanaoingia, baadae ndio mnawapima na kujisifu kwamba mumepima watu wengi.

Nadhani sasa mnafahamu wapi mnapaswa kupeleka nguvu zenu zaidi, muachane na mambo yasiyokuwa na umuhimu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesahau kuwa tutawapiku Wakenya kwa hili janga la Corona.
 
Wiki jana (au juzi) waandishi wawili wa habari wa Kenya walisikika wakimjadili na kumlaumu Rais wetu kwamba anaendesha nchi kama Headmaster. Wakati Kenya na Uganda wanafunga mipaka ya nchi zao, Rais Magufuli hashirikiani na marais wenzake ili Afrika Mashariki itoke na hatua zinazofanana katika kukabili ugonjwa wa corona. Walienda mbali zaidi kumkejeli Rais Magufuli kwamba anawaambia Watanzania wasali kuomba tatizo la ugonjwa wa corona liishe.

Ni kweli Rais wetu alisema tusali; lakini siyo kwamba aliishia penye kusali tu. Alisema wakati tunasali, tufuate pia maelekezo yanayotolewa na serikali: kama kutosongamana; kunawa; kutosalimiana kwa kushikana mikono; waingiao nchini kutoka nchi fulani fulani kuwekwa karantini, n.k. Wanahabari hao walionekana wakimdhihaki Rais wetu kama mtoto mdogo au mwendawazimu anayefanya mambo ya kijinga. Wakaishia kumwita Headmaster anayetoa amri na wananchi wake wanafuata tu kama kondoo. Dhihaka hizi zilinichefua sana. Sasa Wakenya haohao wanakimbilia kwetu kwa Headmaster anayeamrisha mambo ya kijinga.
 
Utakuwa na wadudu kwenye ubongo si bure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao ndio wakenya, sasa umeanza kuwaelewa, kujifanya wanajua kila kitu, kujifanya kila kinachofanyika Kenya ndio sahihi na wengine wote wanapaswa kuiga toka kwao, lakini wao ndio watu wa kwanza kulalamika pale mambo yanapowazidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…