Wakenya acheni utoto

Wakenya acheni utoto

Ni sawa lakini kama unavyojua kuwa mtu anakuwa vizuri zaidi na akiwa amedhamiria kufikisha ujumbe basi hutumia mother tongue yaani first language ambayo nina uhakika kwa wakenya haiwezi kuwa ni English bali lugha za makabila ambazo mtoto anaimasta nyumbani then English shule

Point yangu ni kuwa jamaa kaamua kutumia English ili asikike zaidi maana hiyo language ni lingua franca
Mkuu, Mother tongue ya Kenya ni kiswahili. Vipi lakini ,angeongea kikikuyu wajaluo na wakamba wangemuelewa?
 
Jamii forum ina bahati mbaya kuwa na waanzisha mada kama wewe. Ni kama kitu pekee mnachojivunia ni kuanzisha mada za ujinga zenye maandidhi marefu marefu.

Grow up.
 
Wakenya hawana lolote wanacho kifanya ni MAIGIZO tu.

Ukiona mbongo anasali kwa kiingereza basi jua hana shida huyo.

Ukiona mtu anaelezea matatizo yake kwa lugha ya kigeni wakati ana option ya kuyaelezea kwa lugha yake mwenyewe basi jua hana matatizo huyo.

Muandamanaji anasema

" we are tired. This government is bad. We are hungry. We don't have food " blah blah blah.

And you are taking him seriously?

Angekuwa ana shida kweli angezitaja kwa lugha mama yake na sio lugha ya kigeni.

Upo na matatizo ya ukweli ukweli unapata wapi muda wa kufanya madoido ya kutumia lugha ya kigeni?

Saikolojia ya lugha inayo muhusu mwafrika inasema mwafrika huwaga anataja matatizo yake kwa lugha mama yake na kamwe hawezi kuyataja kwa lugha ya kigeni ambayo huwa mwafrika anaiona superior language.

Jambo zuri atalitaja kwa kiingereza ila jambo baya ndo atalitaja kwa kiswahili.


Mfano Slay queen aliyeibiwa iPhone, hata siku moja hawezi kusema " MY iPhone has been stolen"

Atasema " YESTERDAY I WENT TO BUY AN IPHONE AT MLIMANI CITY, ILA NILIPOPITA MANZESE IKAIBIWA"

So acheni kuwaambia wabongo waige huo utoto wa Wakenya.

Moderator naomba msiunganishe Uzi huu na nyuzi nyingine
Nimecheka sana mkuu.
 
Back
Top Bottom