Wakenya na Kingereza

Bora ubebane na condom.... Hatutaki maambukizi ya Marathi ya ujamaa.
Usijali, Niko fiti, Utafiti unanipa ithibati kuwa kwa kukata Govi naepuka maambukizi kwa karibu 60%, sijui kwa nini Wewe hujakata hilo Govi hadi leo!
 
Jirani huku Kwamtogole tunakijua Kimalkia na sisi tuna watch BBC World News. Unafikiri bado tuko kwenye Things Fall Apart?
Wewe umechanuka sana Skyeclat. Wewe ni wale dotcom. Kizungu unakimanya sawasawa πŸ˜€πŸ˜€
 
Hata sijakuelewa kwani kuwa na ela mfukoni au kuvaa vizuri ndio kujua lugha ya kingereza..?
 
Au kama wewe unakijua ungeandika hii thread kwa lugha ya kingereza kuliko kusifia na kumtukuza mkenya anaeongea kingeleza... (poor thinking capacity)
 
Nadhani ndio sababu pekee Wakenya huchukulia Kingereza kama "Something special" au kitu cha High class, Nashukuru kwa ufafanuzi mkuu.
Kingereza ni special na hata ukisema nini, kitabaki kuwa special. Kimenifungulia milango mingi sana. Kiswahili pia ni muhimu kwa mawasiliano ya kifamilia au kirafiki. Lakini kwa mawasiliano ya kibiashara au kimasomo, itabidi umeongea lugha hio unayoidharau. Usije ukawa kama rais wenu asiyekifahamu king'ong'o halafu sasa anaogopa kusafiri ulaya kuongea na viongozi wenzake, akabakia tu kuzunguka ndani ya mipaka ya nchi yako. Ni aibu kubwa sana hadi masikitiko πŸ™πŸ™πŸ™
 
Tanzania tuna lugha yetu kiswahili kushabikia milugha mingine naona ni uboya na ushamba
 
Nope, Point ni hii, Kenyans brag and feel so proud just for knowing queen's Langage, which to me indeed is just a Language kama tu kihehe cha kwetu. that was my point, note this into your huge empty hollow skull.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] tatizo lenu mkikosa point za msingi mnaishia kutoa maneno ya dhihaka na kutusi.. Tuache hayo..

Hiv kati ya mie na ww nani mfuvu tupu!?[emoji23] [emoji23]
Wewe mwenyewe umesema ulimshangaa mtu wa chini kuzungumza lugha ya malikia, nyinyi ndio wale mapopoma ambao mnaona kingereza ni dalili ya mtu kuwa kasoma sana au ana pesa, ni sisi bongo tu ambao tunaona kiingereza ni lugha ya mbinguni, we mwenyewe umekurupuka na kingereza chako cha kuombea bilauri ya maji london pale, ndio nyie mnobinga kiswanglishi neno moja la kiswahili una mix na kiingereza.[emoji124] [emoji124] [emoji124]
 

Sijaelewa hizo kauli za kwamba Wakenya hatuna lugha rasmi umezitoa wapi, kumbuka Kiswahili kilibuniwa kwenye Pwani za Kenya na Tanzania, kwa hivyo kuna watu kule ndio lugha yao ya asili. Halafu pia fahamu Kiswahili ndio lugha yetu ya taifa hata kwenye katiba kinatambulika rasmi, Kingereza tunatumia kama lugha ya biashara.

Lakini kikubwa, hamna haja ujifunze lugha kisha ugome kuitumia, ndio maana shuleni tunajifuza kingereza na Kiswahili na pia kuzitumia kitaani, maana leo hii ujifunze Kijerumani na hukitumii kitafutika na kukosa umuhimu ndani ya maisha yako.
Kingereza ni muhimu sana kwenye baadhi ya taaluma, unajikuta unatiririka vizuri na kujieleza bila kuhangaika kutafuta maneno.

Nikiwa Bongo nilikua naona Watanzania kwenye vikao wanatatizika sana kujieleza kwa kutumia kingereza, unakuta kikao tupo watu wa mataifa mbali mbali na lugha rasmi humo ni kingereza, sasa Watanzania wanabaki kimya muda wote maana kila anayepewa nafasi ya kuongea anafikia maeneo na kuganda au kujichanganya. Halafu angalia stakabadhi zenu nyingi na sheria mumeandika kwa kingereza, hivyo kwa njia moja au nyingine hamuwezi kukikwepa, wacheni uzembe wa lugha.
 
Kujua lugha zaidi ya moja kuna faida kubwa sana. Hasa lugha za kimataifa. Kuna fungua milango mingi ya maisha. Waingereza wenyewe wanapenda wastoto wao wajifunze Spanish, French au Germany
Uko sahihi, ni vizuri kuzijua lugha tofauti, ila mleta mada kawawakilisha watanzania wengi wenye mtazamo hasi kuwa lugha ya kiingereza ni kwa wasomi na matajiri tu, mtu akibonga ung'eng'e atakuwa kasoma au ana umate mate.
 
Kuna mwalimu wangu alikuwa anasema namnukuu "kujua kuongea kiingereza sio ndo majibu ya mtihani unatakiwa usome ili ujue majibu"
 
Usijali, Niko fiti, Utafiti unanipa ithibati kuwa kwa kukata Govi naepuka maambukizi kwa karibu 60%, sijui kwa nini Wewe hujakata hilo Govi hadi leo!

Mimi nilikata naambiwa nyie hamfanyi hayo mambo.... Ndo akili zenu zimelala hadi leo
 
Endelea kuamini hivyo, Mchina hajui hiyo Lugha na amewaibia kwenye SGR, Kingereza ni Lugha kama zilivyo Lugha nyingine nyie wakenya mbona malofa hivyo miaka yote?
 
Nani aliekudanga kuwa Raisi wetu haajui kuongea kiingereza? Ndo mnavyo danganyana mkiwa kwenye vijiwe vyenu vya githeri sio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…