pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,350
Nimekumbana na habari hizi na video hii pia kwenye kumbukumbu za enzi zile, 'hapa kazi tu' ilipokuwa imepamba moto kweli kweli. Ila nikabaki na maswali chungu nzima baada ya ahadi na kauli hii kunikanganya. Majirani waliambiwa live kwamba Tz itakuwa kama ulaya. Eti na viwanda vya nguo vitajengwa kwa wingi na watz wote watakuwa wanavalia nguo mpya mpya. Huku nguo walizozivalia tayari, yaani mitumba, zitakuwa zinasafirishwa na kuuzwa ulaya.
Hivi hizi ni ndoto roho safi au ni uongo uongo tu wa kuihadaa umma kimakusudi? Kauli kama hizi zinaendana kweli na 'dynamics' za biashara kimataifa, kwa wale ambao wanaelewa taswira ya sekta kusika kule Marekani na Ulaya? Majirani mmekaribishwa pia mtueleze kwa kina kuhusu hii azma yenu. Mmefikia hatua ipi miaka miine baadaye, viwanda tayari?
Vipi kuhusu belo za mitumba kutoka Tz, tayari zipo kwenye soko kule Ulaya?