Sasa nani kakuambia kwamba ni lazima kubargain na usipobargain ni kosa?,. Hiyo ni utamaduni wa biashara, kama unadhani au mumezoea kubargain hakuna anayekukataza endeleeni, na kwa wale ambao hawajazoea kufanya hivyo, pia kwao ni sawa, sasa wewe unaposema " ndio maana biashara inadoda", huo ni kutaka kuamulia watu utamaduni wao wa kufanya biashara.
Hii tabia ya wakenya kujifanya kuwa ninyi ndio 'bench mark" ya kila kitu, ndio inayofanya nchi nyingi ziwe very " uncomfortable' na ninyi. Jaribuni kujishusha kidogo na kuheshimu maisha ya watu wengine, kwa tabii hii mtalalamika sana kwamba watanzania wanawachukia, lakini ninyi wenyewe tabia yenu ya kujikweza ndio chanzo.