Wakenya ninyi ni ndugu zetu wa damu- tunashukuru kwa faraja zenu kwenye msiba wa Magufuli

gango2

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2011
Posts
1,956
Reaction score
2,274
Kwa kweli Kenya na Tanzania ni nchi mbili marafiki sana na niseme ni kama ndugu:

Naona toka msiba huu umetokea Kenya wanauchukua pia kama wao: Mambo yafuatayo yametoa faraja sana kwetu toka kenya

1. Rais Kenya kuhutubia taifa kuhusu msiba wa Rais wetu aliyetangulia mbele za haki Magufuli

2. Kutangazwa siku za maombolezo (nafikiri hili ni kwa mujibu wa EAC)

3. Leo vyombo vyote vya habari kenya vilikuwa vinarusha live matukio ya kumuaga Rais Magufuli

Tofauti kabisa na nchi nyingine za Africa mashariki kama Uganda, Rwanda na Burundi.

Hakika Kenya na sisi ni taifa moja.
 
Wapo waendesha ligi humu kutoka pande zote, Bongo na Genge. Watakuja kulazimisha mabishano yasiyo na tija
 
Kweli hata mk254 wakati wa tetesi za ugonjwa alitoa kauli ya busara hakutaka kukejeli wala kujiingiza kwenye malumbano
 
Na kesho uje uwapongeze wa uganda sawa
 
Ndio desturi ya Afrika, ukiondolea mbali urais, yule alikua baba wa familia, mume wa mtu, kaka wa watu, hivyo muhimu aombolezwe kama binadamu yeyote yule. Pia nilipenda sana ujasiri wake na alivyopenda kujiamini na kusimamia maamuzi yake, yaani tu angekua anakubali kushauriwa, yule angekua rais wa kuigwa dunia yote.
Hapo pakugomea ushauri huwa namfananisha na marehemu babangu, hawa ni wazee wale ambao walikuzwa kwenye desturi zenye dhana kwamba mzee haambiwi wala kushauriwa, yaani babangu ilikua ukitaka kumshauri au kumpinga ujiandae kupokea kibao.

Haka kaugonjwa kamebadilisha tunavyoishi na kuhusiana, maana hata misiba kwetu huku Kenya hatuhudhurii, tunabonyeza tu Mpesa na kutuma michango na kuwaachia ndugu wa karibu wazike wao.
Hapa tayari tumetaarifiwa kuna corona v3 ambayo inakuathiri kimya kimya, yaani dalili utazihisi siku unapukutika, hivyo vile vipimo sijui vya joto wala nini havisaidii tena. Itabidi serikali iharakishe hii chanjo la sivyo "twafwa".
 
Watanzania hatuna shukurani, hata tufanyiwe nini haipiti muda tunaanza wehu wetu. Halafu tukipigwa spana za vichwa tunaanza kujilizaliza.

Juzi tu huyu wanaotusaidia kumlilia aliwakamata wamama wa kimasai border ya tanzania kuchunga ng'ombe na kuwachapa fine kila mtu ameizing. Halafu mkuu wa mkoa yalimtoka maneno ya shombo kuhusu hao kina mama wa kimasai kwamba hawana passport wala document za immigration.

Kumbuka mwaka jana, Namanga, afisa immigrarion alichoma moto vifaranga vya kuku 5,000 vikiwa hai, badala ya kuvirudisha kenya vilipotoka.

Mwaka jana huo huo, Kenya Airways zilinyimwa ruhusa ya kutua Airport za Tanzania.
 
To be fair mara nyingi hizi chokochoko wanaanzisha wakenya kuliko watanzania.
Kenyatta alianza kufungia ndege kutoka Tanzania alichofanya magufuli ni reciprocal action hakuna alichoongeza.

Pia huwezi kuchunga ng'ombe nchi jirani bila ruhusa kumbuka kutokujua sheria sio utetezi.

Kuchoma vifaranga lilikuwa kosa kweli.
 
gango2 Sema Wakenya ndugu zako wewe!
Hawa wapumbavu sijui wanafikiria kwa kutumia kiungo gani, eti kujiunga na tbc ndio undugu tayari

Wasubiri baada ya kujiunga na tbc waone ktn inavyompigia simu lissu waanze kumtukana Magufuli na Tanzania
Hatuna undugu wowote zaidi ya ujirani wa bahati mbaya
 
Hawa wapumbavu sijui wanafikiria kwa kutumia kiungo gani, eti kujiunga na tbc ndio undugu tayari

Wasubiri baada ya kujiunga na tbc waone ktn inavyompigia simu lissu aanze kumtukana Magufuli na Tanzania
halafu unajua KTN ni media ya Moi family!
 
Hiyo TV na nyingine zote Kenya huwa wanamuhoji lissu tu kumuelezea Magufuli ni wa aina gani, wachambuzi wao wote kwenye programs zao wanamuongelea Magufuli vibaya sana kupita maelezo yaani hata jema 1 tu hana.

Nawashangaa hawa Nyumbu wanafikiri kujiunga na tbc ndio undugu
 
Wakitumia super infrastructure za Azam media na TBC!
 
Ndio desturi ya Afrika, ukiondolea mbali urais, yule alikua baba wa familia, mume wa mtu, kaka wa watu, hivyo muhimu aombolezwe kama binadamu yeyote yule. Pia nilipenda sana ujasiri wake na alivyopenda kujiamini na kusimamia maamuzi yake, yaani tu angekua anakubali kushauriwa, yule angekua rais wa kuigwa dunia yote.
Hapo pakugomea ushauri huwa namfananisha na marehemu babangu, hawa ni wazee wale ambao walikuzwa kwenye desturi zenye dhana kwamba mzee haambiwi wala kushauriwa, yaani babangu ilikua ukitaka kumshauri au kumpinga ujiandae kupokea kibao.

Haka kaugonjwa kamebadilisha tunavyoishi na kuhusiana, maana hata misiba kwetu huku Kenya hatuhudhurii, tunabonyeza tu Mpesa na kutuma michango na kuwaachia ndugu wa karibu wazike wao.
Hapa tayari tumetaarifiwa kuna corona v3 ambayo inakuathiri kimya kimya, yaani dalili utazihisi siku unapukutika, hivyo vile vipimo sijui vya joto wala nini havisaidii tena. Itabidi serikali iharakishe hii chanjo la sivyo "twafwa".
Sasa si watangaze tu hivi virusi vinafanana na vya ngoma sababu hii ni mara ya tatu sasa vinabadilika. Kitu ambacho sijajua ni je kila vinavyobadilika inabidi uchome chanjo mpya kama ilivyotokea south africa au inakuwaje? Na kama inabidi uchome kila vinavyobadilika sasa kwanini wasiwekeze kwenye dawa za kuponya kuliko hizo chanjo?
 
Back
Top Bottom