Wakenya tumwombee mwanzilishi wa Jamii Forums

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Kuna taarifa kwamba mwanzilishi wa Jamii Forums ambaye ni mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, kampuni inayomiliki mtandao wetu huu maarufu wa Jamii Forums, Maxence Melo, amekamatwa na kushtakiwa kwa kugoma kutoa majina ya watumiaji wa huu mfumo. Nafikiri sheria ya Tanzania ilibadilishwa kwamba kila mtandao wa kijamii unahitajika kutoa majina na taarifa za watumiaji wake.

Hapa ni kwa sisi Wakenya wanachama wa JF, na hata Wabongo tunaokutana nao kila siku kwenye Kenyan section ya JF kuomba busara kutumika ili mambo yafanyike bila kufikia hatua au maamuzi ya huu mtandao kupigwa chini, maana kwa sasa upo maarufu Afrika Mashariki, sote tunakutana humu, tuna wachangiaji kutokea Rwanda, Kenya na hata Nigeria. Kwa kifupi tumekua jamii moja, ukiweka pembeni utani wa kutambiana.

Lakini pia tunafaa kuheshimu dola na mamlaka zetu, anyway kweli tumwombee Max.

NEWS ALERT: mwanzilishi wa Jamii Forums Maxence melo ashikilwa na jeshi la polisi, kupanda kizimbani leo | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today
 
Mk254 ,usije ukaombea na wengine ambao hawahusiki,naomba maombi yawe kwa mello tu.
 
Amin !!
images
 
Tatizo jamii forum inaangaliwa kwenye makosa tu hawaoni faida zake ,mfano ishu ya yule Binti wa Raila Odinga aliyesema Oldupai Gorge ipo Kenya kwa umoja wetu tulipinga upotoshaji ule wa wazi

Au ishu ya Museveni kutaka kutumia bandari yetu ya Tanga ,ninyi Wakenya mkafanya lobbying zenu na propaganda kibao mpaka kumuingiza sijui kiongozi gani kwenye Chopa ambaye hakuwepo kwenye manifest kutembelea bandari ya Tanga ila kwa umoja wetu tulitetea hilo na maafisa uhamiaji walimzuia

Ukiacha na mitambo ya hapa na pale sisi na Wakenya ni ndugu
Wakifunga forum hii sijui ni nini kitatuleta pamoja
 
Ila ole wako uzungumzie kivuko kwa kwenda Ununio, hapa watazaa na wewe. Ogopa kama ukoma watu wanaopenda kusifiwa tu na sio kukosolewa. Ogopa kweli kweli.
 
amina mkuu kweli hapa yatupasa kuwa wamoja
ila sirikli yetu haiyaki kusikia ikisemwa pale inapochemka
kwa baadhi ya mambo.
 
Tatizo jamii forum inaangaliwa kwenye makosa tu hawaoni faida zake ,mfano ishu ya yule Binti wa Raila Odinga aliyesema Oldupai Gorge ipo Kenya kwa umoja wetu tulipinga upotoshaji ule wa wazi

Au ishu ya Museveni kutaka kutumia bandari yetu ya Tanga ,ninyi Wakenya mkafanya lobbying zenu na propaganda kibao mpaka kumuingiza sijui kiongozi gani kwenye Chopa ambaye hakuwepo kwenye manifest kutembelea bandari ya Tanga ila kwa umoja wetu tulitetea hilo na maafisa uhamiaji walimzuia

Ukiacha na mitambo ya hapa na pale sisi na Wakenya ni ndugu
Wakifunga forum hii sijui ni nini kitatuleta pamoja
tunambiwa maombi bado upo kwa ligi
 
MK254 katika ubora wako! Tusisahau pia misa ya kumuombea marehemu Jacob Juma.

Masunga Maziku
Jacob Juma kama ni yule namfahamu, huyo tayari ni maiti na keshazikwa hivyo maombi yetu kwake hayatakua na umuhimu.
Huyo aliuawa kinyama jameni, kumekua na tetesi system ya serikali ilihusika.

Anyway hii mada inamhusu mumiliki wa huu mtandao wetu wa JF maana kama vipi ukipigwa chini basi hatutakua hata na fursa ya kuagana.

Sipati picha jamii ya watu 300,000 sote tukipoteana ghafla. Tumuweke kwenye maombi.
 
Back
Top Bottom