MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Kuna taarifa kwamba mwanzilishi wa Jamii Forums ambaye ni mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, kampuni inayomiliki mtandao wetu huu maarufu wa Jamii Forums, Maxence Melo, amekamatwa na kushtakiwa kwa kugoma kutoa majina ya watumiaji wa huu mfumo. Nafikiri sheria ya Tanzania ilibadilishwa kwamba kila mtandao wa kijamii unahitajika kutoa majina na taarifa za watumiaji wake.
Hapa ni kwa sisi Wakenya wanachama wa JF, na hata Wabongo tunaokutana nao kila siku kwenye Kenyan section ya JF kuomba busara kutumika ili mambo yafanyike bila kufikia hatua au maamuzi ya huu mtandao kupigwa chini, maana kwa sasa upo maarufu Afrika Mashariki, sote tunakutana humu, tuna wachangiaji kutokea Rwanda, Kenya na hata Nigeria. Kwa kifupi tumekua jamii moja, ukiweka pembeni utani wa kutambiana.
Lakini pia tunafaa kuheshimu dola na mamlaka zetu, anyway kweli tumwombee Max.
NEWS ALERT: mwanzilishi wa Jamii Forums Maxence melo ashikilwa na jeshi la polisi, kupanda kizimbani leo | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today