Ubaguzi wa kikabila chanzo chake sio lugha, hili nimelisema mara nyingi. Somalia kule wanaongea lugha moja, dini moja lakini wanauana na kubaguana kwa misingi ya kiukoo.
Kenya, kuna sababu chache zilizotuponza hapo awali ndio vikasababisha ukabila, japo tunajaribu sana kupunguza.
- Muingereza alizoea kuwagawa mababu zetu kwa misingi ya kikabila hata kabla ya uhuru, yaani divide and rule. Hivyo wakati anatuachia nchi, alikua tayari keshaachia sumu na mbegu ya ukabila imezagaa. Lakini Tanzania mambo yalikua tofauti, kwanza Muingereza aliwatawala akijua ataachia hivyo hakua na sababu za kung'ang'ania nchi yenu na akawaacha muishi bila vita au ugomvi wowote baina yenu.
- Pili, Muingereza wakati anaachia Kenya, alikabidhi uongozi kwa mtu wa kutokea kwa kabila kubwa, kabila langu la Wakikuyu. Hilo lilichangia pia, maana kwenu kaachia kwa mtu wa kabila ndogo sana, Mzanaki. Lakini angeachia uongozi kwa mtu wa kabila kubwa mfano Wachagga, mungekoma.
Zaidi nataka kusema, ubaguzi ni asili ya binadamu, huwa lazima tubaguane kwa njia moja au nyingine. Kwa mfano hapo Bongo mnabaguana sana kwa misingi ya kidini, hilo nimeona hata video za masheikh wa kiislamu wakilalamika balaa.
Ubaguzi mwengine ambao upo duniani kote ni wa baina ya matajiri na maskini, walio nacho na wasiokua nacho. Huo upo Bongo, Kenya na hata Marekani.