Wakenya tushukuru Mungu kwa demokrasia yetu, watani wetu wamebanwa hadi wanalia toshaaa, wanakiri kwamba nchi yao sasa imekuwa 'Police State'

Wakenya tushukuru Mungu kwa demokrasia yetu, watani wetu wamebanwa hadi wanalia toshaaa, wanakiri kwamba nchi yao sasa imekuwa 'Police State'

ni kweli kabisa Tanzania inapitia wakati mgumu sana katika historia ya taifa lefu
Boss umebofya hiyo link hapo na ukasoma taarifa yenyewe? Au umetangulia tu kutupia comment ya kishabik? Hii ni sifa mbaya sana kwa nchi yenu. Wakenya tumeishi kwenye hali kama hiyo ya 'police state' chini ya utawala wa rais mstaafu Daniel Arap Moi, almaarufu Nyayo. Usitamani kuyaona yale ambayo sisi tuliyashuhudia. Wazazi wetu wakivamiwa usiku wa manane na kuzabwa makofi, huku wakinyanyuliwa juu kwa juu na kutupwa kwenye landcruiser na kutawacha tukijiuliza kama ndio itakuwa siku yetu ya mwisho ya kuwaona kwa macho yetu mawili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
haya wakenya nyingine hii hapa,imagine hapo kenya jubilee ilazimishe primary school students kwenda kusafisha office zake then mtu wa ODM akataze mwanaye halafu district commisoner anaamrisha police wamkamate,hiyo ndiyo NEW TANZANIA najua hamuamini ila ni disaster kwa kifupi tumekatika tumegawanyika kama nchi kuna watoto wapendwa yaani ccm na step kids yaani opposition, ni mateso makubwa tribulation ndugu zetu ,kenya mnayo matatizo yenu tunajua ila sisi tunapoeleka itakuwa the worst tunaongozwa na kichaa a.k,a jiwe,hawezi kushindana hawezi ku argue,ni muoga wa challenges anapenda kusifiwa tu hadi hesabu za serikali anaficha hamtaki CAG sababu anafichua madudu,so far 1 billion dollars hazijulikani zimetumikaje
View attachment 1067271
Hahahahaha this one is ludicrous .LOL..
Mtoto wa Wyatt Mathewson aliona cha mtema kuni 😆😆😆
 
Umesoma uzi? Umeelewa??

Usini quote kama huwezi kusoma na kuelewa. Elewa kwanza, jenga hoja, jikite wenye mada.
Dude, de other guy asked, JPM ameficha nini? Ukamwambia watu kama yeye ni wajinga ndio wametufikisha hapa, nikakuuliza hapo wapi, ukaanza singizia soma uzi.
Kama JPM kaficha, ungeona wapi hizi reports za CAG? Na unajuaje wewe sio ze mjinga one.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii nayo ni hatari, Civil Society Organisations Director's Forum ambayo ni mkusanyiko wa mashirika 65 ya kitanzania ya haki za kibinadamu na kidemokrasia limeamua kupaza sauti liwe liwalo. Wanalalamika na kulilia dunia kwa kile ambacho wanakiita 'Police State' ambayo mzee mtakatifu kule ikulu ameibuka nayo kwa kukandamiza kabisa upinzani, wanahabari na uhuru wa wananchi wake. Wanasema kwa mwendo huu wa kuminya demokrasia na uhuru wa wapinzani kuwa na vikao vyao, amani ya nchi inavurugwa huku katiba ikinajisiwa na viongozi wanaotawala. Matokeo yake ni wananchi wanaoishi kwa uoga na kujihisi kwamba hawapo huru kwenye nchi yao. Wameangazia sanasana kutupwa selo kwa miezi mitatu kwa kiongozi mmoja wa upinzani, Mr. Freeman Mbowe. Kunani watani wetu watanzania? Mnanikumbusha enzi za Nyayo Kenya. Mbona mmebadilika kiasi hiki? Tuliwajua kwa ustaarabu wenu ila sasa sivyo tena. https://www.africanews.com/2019/04/...n-groups-risks-undermining-peace-in-tanzania/
Ni kweli kabsaaaa
 
Bull shit post

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom