Asante kwa kuniita japo sioni chochote cha kuchangia hapa, maana labda Mkenya bogus anaweza kukimbilia kuja kwa nchi ambayo yenyewe kwa umaskini imelemewa na zoezi la kuendelea kupima watu wake mpaka kunatokea matukio ya raia wake kutokea Tanga kwenda kuambukiza Zanzibar, ikikumbukwa Tanga haijawahi kutajwa popote wakati mlikua mnajitutumua kupima.
Ni wazi kwenu huko kirusi kimezagaa sema ni ile kwa Afrika hakiui wala kuathiri sana, hivyo hata kikiwa mtaani ni vigumu kujua kama ni chenyewe, hii mpaka sasa inajadiliwa na wataalam imekuaje Afrika vifo ni vichache sana. Kuna Watanzania wanajiaminisha waliwahi kuumwa Corona, hebu fuata huu uzi
Kwa tulioumwa mafua yale ni mashahidi tosha, nahisi ile ilikuwa ni Covid 19 - JamiiForums
Halafu hizi taarifa nahisi zimekaa kipropaganda zaidi, hata kama ingekua kuna Mkenya anatoroka, labda atoroke kutoka Nairobi maana kesi 82% ni za Nairobi, kwingine mamilioni ya Wakenya wanasoma tu kwenye magazeti wala hawana habari, sasa iweje Mkenya wa huko karibu na Sirari atoroke nchi.
Ndio maana Nairobi na gatuzi kadhaa za Pwani zimeongezewa curfew zaidi.