Off point, tatizo lenu wakenya hampendi kujifunza kwa waliofanikiwa kutokana na kiburi chenu cha kujifanya mnajua kila kitu.
Hakuna ubishi kwamba Tanzania tumefanikiwa kutokomeza ukabila, Hakuna ubishi kwamba kwa kutumia lugha moja ya Kiswahili nchi nzima, ni miongoni mwa sababu kubwa katika kutokomeza ukabila, kwanini msiige hilo?.
Nani aliyesema Tanzania tunadharau lugha za asili?, humsikii Magufuli akizungumza baadhi ya maeneo, kama tungekua tunazidharau asingezungumza.
Huko vijijini huwa tunazungumza lugha zetu kwasababu zaidi ya 98% ya wakazi huko vijijini wanaelewa hiyo lugha, kwahiyo hakuna hatari ya watu kujitenga kutokana na "language barrier".
It is very uncivilized" kuzungumza lugha ambayo nusu ya watu waliopo hawaelewi hiyo lugha, hasa katika ofisi za serikali na public places. Hivi kweli unaingia ofisini au Hospitalini unakuta Daktari mkikuyu anazungumza Gikuyu na baadhi ya Nurses ambao ni wakikuyu, Daktari mjaluo anazungumza Kijaluo na Nurses wa kijaluo, eti kwasababu wanalinda Mila na desturi zao, Nonsense.
Kuhusu wanaoandika kumkashifu Prof. Ngugi, muhimu sio idadi ya watu wangapi wameandika, muhimu ni kilichoandikwa, ukisoma wote walioandika wanazungumzia umuhimu wa Lugha katika kuunganisha nchi.
Unapozungumza lugha inayoeleweka na watu wengi, kunasaidia kuunganisha jamii, lakini unapotumia lugha ya jamii moja na kuacha kundi kubwa, huko ni kutenga na kuigawa jamii husika.
Umuhimu wa Kiswahili ni
1)Ndio lugha inayoeleweka kwa watu wengi zaidi Kenya
2)Hakuna kabila lolote katika Afrika au Kenya ambalo linahodhi au kumiliki Kiswahili
Kwahiyo Kiswahili kinaunganisha watu wa Kenya na kinaeleweka kwa wakenya wengi bila kujali makabila yao.
Tumieni Kiswahili ili kuleta wakenya pamoja na kupambana na ukabila. Acheni kuendekeza ukabila kwa kisingizio cha kulinda mila na desturi, huo ni upumbavu na ni hatari Sana.