Wakenya wametupiga bao sana kwenye uwekezaji nchini

nataka nikawekeze kenya katika kilimo cha vitunguu naomba muongozo.
 
Kama ndiyo tunategemea CCM ituvushe tusahau
 
Tz ni nchi ya ajabu Sana narudia ni nchi ya ajabu Sana , viongozi wengi wapo outdated hasa kwenye masuala ya finance , Kenya wametoboka Sana nje ,na kule wanapata exposure wakija wanawekeza vtu vizito , bank Tu kama KCB na equity zinakimbiza hatari , Sisi ni hovyo hovyo tuuu , mpak Leo malipo ya PayPal hayafanyiki tz, kupata hela mpak upitie Kenya what the fuc-k , hii nchi sjui ina laana gani ,mtu kusepa nje unawekewa vikwazo kibao yaan ....
 
kenya wamewekeza vitu vidogo dogo kama maduka ya madawa na bar nkTanzania kampuni chache lakini za nguvu
Ukiona hivyo, jua ni rahisi kuwekeza Tanzania.
Yaani ninyi !!. Mungu awasamehe bure tu, hamna namna [emoji102]. Siasa zetu zimekuwa na athari mbaya kwa nchi na wananchi wake. Hiyo ya kwenu ni uzalendo uchwara
 
Sijui Wakenya wanatoa watu wapi?wa kuwatetea na kuthamini vitu vyao.Huu mtindo wa Ovyo kabisa kuwahi kutokea.
 
Hivi unaweza kuziorodhesha kampuni hizo 529 ,mkuu, ili tujue na tuweze kuchangia vizuri mada yako?

Najuwa wapo Kampuni ya Agha Khan, ile ya magazeti, yapo mabenki kadhaa, kama DiamondTrust Bank, KCB, na ile ya James Mwangi, Equity Bank; haya tunayafahamu vizuri na tunaweza kuyaongelea bila ya matatizo.

Kuna mengine ya Bima, kama AAR, iliyotangaza hivi karibuni kufungasha vilago, nayo inaitwa ya Kenya?

Kwa ufupi mkuu, tafadhali tuwekee hiyo orodha kamili hapa tupate kuijadili vyema.

Ni makampuni yapi ya Kenya yaliyowekeza Tanzania? Hili ni swali muhimu, lijibiwe.

Tukianzia hapo, tunaweza sasa kulinganisha uwekezaji kwa mwenzake kati ya nchi hizi mbili.
 
Waje tu, watupatie hata kazi za ulinzi na kusafisha ofisi na kuwaoshea magari

Maana sisi tumezubaa tu.
Hii ni hoja muflisi kabisa...!
Sema waje tujifunze kutoka kwao ili na sisi tupate mwanga katika uwekezaji.

Kama umeshindwa wewe wekeza hayo mawazo kwa mwanao

Jiulize swali hili, "Wao wameweza, kwanini sisi tushindwe?"
 
Mkuu watu elfu 56 kwenye watu zaidi ya milioni 50 ?Acha kuwakuza kwa kiwango hiko huo uwekezaji ni wa kawaida sanaaaaaaa
 
Kama tunachoma vifaranga vyao je?
 
Mkuu makampuni mengi ni ya uchochoroni, ambayo Yana fahamika hayazidi ata 50, anaweweseka na makampuni ya kulipa watu laki na nusu ahahahahahaha
 
Kwanini sisi waTZ tunapenda kujifariji hivi?!!!
Watanzania tujifariji? unaota tukiamua ku compete wakenya watatafuta pa kujificha.Wakenya wakibisha wamuulize Akamba bus service ambaye kenya ndio giant namba moja kwenye usafiri wa mabasi Alijaribu kuleta mabasi ya route ya kenya Tanania alipigwa mateke na Wenye mabasi watanzania wenye mabasi ya Tanzania kwenda kenya akina Dar express nk hadi akafunga ofisi akarudi kwao kenya kwa kushindwa competition.

Hadi leo mabasi ya watanzania ndi yanatamba route ya Tanzania kwenda kenya na kurudi.Wakenya walikimbia mbio

Shahidi Akamba Bus service wa Kenya
 
Wenye mabasi kavamieni soko la kenya .Nairobi nk bado wanatumia vipanya kama daladala pia safari za mikoa mibus ya hovyo na vipanya vinaenda mkoa hadi mkoa maeneo kibao .Mabasi mazuri machache hasa ya kutoka Nairobi kwenda mikoa mingine ya kenya.Mazuri ni ya Mombasa Nairobi tu

Abood bus sevice ,Sauli nk kaavamieni soko la ndani kenya
 
Hata sisi tumewapiga bao kwenye uzinzi, ulevi, uvivu, utapeli na ushirikina.
Sisi biashara lazima tupende kusoma na kujifunza. Sisi lazima tutambue kwamba bila dhamira yetu wenyewe ya kutafuta maendeleo, hatutaendelea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…