Wakenya wametupiga bao sana kwenye uwekezaji nchini

Wakenya wametupiga bao sana kwenye uwekezaji nchini

Unachekesha,kuanzia leo jua kwamba gap imeongezeka hizo ndoto za kuwakuta sahau,Ghana walikuwa nyuma yetu leo vipi?

Pili kusaport private sector unajua ni kufanyaje? Ni pamoja na kuondoa vikwazo vya biashara na kuwa na kodi rafiki.

Nchi hii haieleweki siasa yake kwenye swala la uchumi na tuna viongozi ambao hawawezi kusupoort biashara.mfano wakati kuna mzozo wa biashara Kati ya Kenya na Tzn ,,wanasiasa uchwara kila mtu alikuja na tamko na kujitutumua ikaishia kutupa hasara
Kwenye kulaumu serikali nakumbuka wewe ulikuwa ni kinara sijui kama siku hizi umeacha ulikuwa ni utoto tu unakusumbua!
 
Nakumat si ndo wakenya na vaseline sabuni za jamaa...sisi tuna akina bakheresa Mo n.k tuwape nguvu tununue vyakwetu. Madini tuwe nayo machooo otherwise mwendazke tutamkumbuka alikuwa anakuja vzr sana
 
Naomba Watanzania Muwekeze Northern Kenya Tafadhali Huko Hapajaguzwa,and Mkiguza sai one day you will be the Billgates of Kenya,Mandungu zangu
Hii northen Kenya tatizo ni miundo mbinu ns usalama ni duni,Alshabab imesumbua muda sasa.
 
Wakuu

Kenya ina jumla ya kampuni 529 zinazoendesha shughuli zake nchini Tanzania ambapo zimewekeza Dola za Marekani Bilioni 1.7 na zimeajiri watu 56,260.

Tanzania sisi sasa tuna kampuni 30 tu. Je, tumekwama wapi kama Nchi?

Nini kifanyike? Waalimu, Wahudumu katika hoteli nyingi ni Wakenya. Wapi wizara zetu na wale watoa maamuzi wanaweka mkakati wa pamoja juu ya hili?
Sasa, Watanzania wataenda kenya kuwekeza nini 😐😐asilimia kubwa ya uchumi wa Kenya umeshikiliwa na wazungu, Makampuni mengi niya wazungu Wakenya ni vibarua, kwenye aridhi ndio usiseme,imeodhiwa na wakubwa,Kiujumla Kenya ni Madarali wa Wazungu, Mtanzania kuweza Kenya ni kujitafutia matatizo tu amna furusa.
 
Kenya ina jumla ya kampuni 529 zinazoendesha shughuli zake nchini Tanzania ambapo zimewekeza Dola za Marekani Bilioni 1.7 na zimeajiri watu 56,260.Hayati Rais Magufuli Tarehe 31 Oktoba, 2016

Tarehe 4 May,2021 Rais Samia Suluhu Hassan. Kenya ina jumla ya kampuni 513 zinazoendesha shughuli zake nchini Tanzania ambapo zimewekeza Dola za Marekani Bilioni 1.7 na zimeajiri watu 51,000.kati ya makampuni 30 tu ya Tanzania yakiwekeza Ksh Bil 19.3 yaliyotoa agira 2600 tu

Mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Kenya iliongezeka kutoka Shilingi za Kitanzania Bilioni 652.9 hadi Shilingi za Kitanzania Trilioni 2.044

Tatizo ni nini Kwa Watanzania,Nini kifanyike,Tunakwama wapi?
Kenya ina jumla ya kampuni 513 zinazoendesha shughuli zake nchini Tanzania ambapo zimewekeza Dola za Marekani Bilioni 1.7 na zimeajiri watu 51,000.kati ya makampuni 30 tu ya Tanzania yakiwekeza Ksh Bil 19.3 yaliyotoa agira 2600 tu
Tatizo kuwekeza Kenya au watanzania kumiliki kampuni?
 
KENYA YUKO TU MBELE YA PAZIA UJUE KUWA NYUMA YA PAZIA HIZO ZOTE NI KAMPUNI ZA U.S.A NA U.K ZILIWEKEZA MITAJI KENYA WAKATI ZIKISUBILIA UJAMAA UANGUKE TANZANIA ULIPOANGUKA NDIO ZIKAVUKA MPAKA. FAIDA KWA WAKENYA NI KUWA ZILIWAPATIA UJUZI WA KUSIMAMIA MAKAMPUNI SASA BAADA YA KUJA TANZANIA HAZIONI SABABU YA KUIGIA TENA GHARAMA KUTOA UJUZI KWA WATANZANIA BALI WALETE WAKENYA WAKASIMAMIE KAMPUNI ZAO NA HAPA SERIKALI YA TANZANIA NDIPO INATAKIWA KUWA MACHO KWELI KWELI
Unajifunza leo kuandika?
 
Tz ni nchi ya ajabu Sana narudia ni nchi ya ajabu Sana , viongozi wengi wapo outdated hasa kwenye masuala ya finance , Kenya wametoboka Sana nje ,na kule wanapata exposure wakija wanawekeza vtu vizito , bank Tu kama KCB na equity zinakimbiza hatari , Sisi ni hovyo hovyo tuuu , mpak Leo malipo ya PayPal hayafanyiki tz, kupata hela mpak upitie Kenya what the fuc-k , hii nchi sjui ina laana gani ,mtu kusepa nje unawekewa vikwazo kibao yaan ....
Wewe sio unaona hata kuwapatia wananchi wake urahisi, wa kuweza pata passport ya kusafiria kwenda nje ya Tz kuweza ku explore fursa na kupata exposure ya wengine wanafanya nini, imekuwa vikwazo vingi kama nchi za kikomunisti. Kwa hiyo sidhani ukategemea kirahisi utaweza shindana na wa Kenya ambao kitambo,wameweza kujaribu kusambaa duniani kote kutafuta fursa za kiuchumi....Sie nasi tujaribu, ilimradi tuwe serious na sio maneno tu bila nia thabiti. Kazi iendelee.
 
Moja.unawekeza kwenye fursa kuangalia kwenye afika mashariki kati ya tanzania na Kenya,tanzania ina fursa nyingi zaidi kuliko Kenya.
Pili,idadi kubwa ya wawekezaji wa Kenya ni rais wa kigeni na "familia kubwa za kikenya" hii kutokana na ain ya maisha walivyo yachagua tangu uhuru.
Tatu,hakuna bepari asieisapoti mtu wake kwenye uwekezaji lakini uwekezaji you use wa kimkakakti je unadhani kimkakakti kuna kitu ambacho tanzania nilitaka ambacho kipo Kenya?
Nne,je kuna sera ya kuwawezesha wazawa wapate exposure kwenye kampuni za wagen za uwekezaji nchini?
HITIMISHO,soko la ndani ni bora zaidi kuliko is jirani,wazee walisema tumbo ya mbali haina nyoka...anza kuja nyoka na tumbo ya karibu mpaka kumaliza tumbo za karibu basi na nyoka wako mbali unaanza kutumia tumbo za mbali ukiwa nyoka wa mbali.
 
When it Comes to Aggressiveness in Business To be Frank Kenyans WAMETUZIDI.
- The Reason is Clear. Bcz After After Independence Tz took Ujamaa Policy which is Non Hostile .
While Kenya took Ubepari na Ukabaila.
Which takes the Form Fit for the Fittest. Belligerent and Struggling.
  • The Result is as what is Seen Now, When it Comes to Private Sectors.
  • Tanzanians may Face a Bit of Hostility when Trying to set up Business, But Gradually with Government Protection, Future Equity is Possible.
Hiyo hawezi kuwa sababu. Ujamaa wa kisera ndio tatizo ila ujamaa wa kijamii si jambo baya. Kwasasa Tanzania hali iliyopo ni tuna ujamaa wa kijamii.

Ila kiuchumi tayari tumeshakubali matokeo kuwa haiwezekani kuendesha taifa letu kwa misingi ya uchumi wa kicommunist na siasa za kicommunist sababu kwa idadi ya watu iliyopo serikali haiwezi kusimamia kila kitu.

Kwa Tanzania ugonjwa uliobakia ni wasiasa uchwara na vyama vyao vya siasa vinavyojikuta vina uphold sera za ujamaa ile hali wananchi ndio wanatakiwa kuwa wajamaa ila sio uchumi.

Vijamaa vinafanya hivi ili viendelee kula mema ya inchi nyuma ya pazia. Vinakataza wawekezaji ili vyenyewe na watoto wao ndio wafungue makampuni uchwara wapige pesa kitapeli.

Ndio maana vingi unaona vinawekana na koo zao katika uongozi, baba, mama, watoto, wajukuu, baba wadogo, wajomba, mashangazi woteeee unawakuta katika mashirika ya serikali.

Tukijua namna ya kuwadismantle hawa katika uongozi na kubadili vifungu kadhaa, ujamaa watu bado tutakuwa nao kijamii huku sera za kibiashara na uchumi tunaoperate kwa kanuni za soko huria bila wasi wasi.
 
Wakenya wana uchumi mkubwa zaidi yetu, pia wana wataalamu wa viwango zaidi yetu sababu elimu yao ni bora, na sio hapa kwetu tu, hao jamaa wametapakaa mpaka SA huko wana exposure ya biashara na wanaongoza mashirika na kampuni, kutaka sisi tuwe kama wao itachukua muda kidogo, nionavyo bora tujifunze toka kwao ili baadae na sisi tuendeshe mambo yetu.

hizi story sjui elimu bora ifike mwisho sasa, kwan hakuna wanaoenda kusoma nje ya nchi? wanatafauti gan na ambao hawajaenda nje? kwan wakina bilgates walimaliza shule? does that conclude elimu yao ni mbaya? enough of this story!
 
Siasa na udalali wa kisiasa
Umalaya wa kisiasa
Kazi ya uchuuzi wa bidhaa
Udalali
Boda boda
Uvivu na kuishia makanisani badala ya kufanya kazi.
Roho mbaya
Hasad
Fitina
Uongo
Uzushi
Wivu

Saa ngapi wabongo watawekeza kwenye nchi nyingine?
 
Wakenya ni mabepari hivyo wao kutafuta zaidi kutanuka iko damuni sio sawa na sisi tunaopenda sana kukaa nyumbani hata kama fursa zimebana au zimetanuka nje ya taifa letu.

Hakuna mtu aliyefanikiwa sana kimaisha kwa kutegemea ndugu zake tu lazima uwe na jicho la tai mbele uwatumie hata usiowajua ndipo utafaidika

sasa watu wenyewe wanalilia ajira miaka nenda rudi makampuni yanaanzishwa mda gan
 
Wkaenyawanavipaji vingisana kuliko TZ
Sisi tumeweka Siasa za maji taka mbele.
Watanzania ni wajuwaji sana ,lakini kielimu tupo chini mno.
Hata hivyi ,hizo biashara zinazosifiwa ni za Wakenya mnajuwa ni wakenya wa jamii ganiwaliowekeza zaidi?
Mii nadhani Wahindi na pengine Wasomali,
sisi Waswahili tunasubiri Vibarua tuu.
Mitaji yetu midogo , Business management zetu ni Poor.
Mswahili kabakia mtu wa Kutumwa tuu na Kulipwaga mishahara.
Hivi mnafahamu kuwa Taasisi moja ya Elimu huko Ulaya ilifanya tamasha kumkumbuka Prof Beno Ndulu na mchango wake katika uchumi alipokuwa UN,Raisi Kikwete alialikwa kwenye huo mhadhara.
 
Siasa na udalali wa kisiasa
Umalaya wa kisiasa
Kazi ya uchuuzi wa bidhaa
Udalali
Boda boda
Uvivu na kuishia makanisani badala ya kufanya kazi.
Roho mbaya
Hasad
Fitina
Uongo
Uzushi
Wivu

Saa ngapi wabongo watawekeza kwenye nchi nyingine?

summarize yote na uconclude kwamba we are lazy, sjawahi kutana na mkenya anaengangania serikali, ukiachana na matatizo yote wanayopitia hawajaacha kutafuta fursa sehem ingine uku wimbo ni ule ule miaka nenda rudi wa ajira serikalini.. wtf!
 
Watu wengine wa ajabu sana. Huku tunahimiza nchi za nje wake kuwekeza. Wakija (Kenya) mnasema tumepigwa. Mbona hamsemi hivyo kuhusu uwekezaji wa UK, South Africa au Mauritius? Magufuli aliharibu sana ajili za watu!
Wakenya wana uchumi mkubwa zaidi yetu, pia wana wataalamu wa viwango zaidi yetu sababu elimu yao ni bora, na sio hapa kwetu tu, hao jamaa wametapakaa mpaka SA huko wana exposure ya biashara na wanaongoza mashirika na kampuni, kutaka sisi tuwe kama wao itachukua muda kidogo, nionavyo bora tujifunze toka kwao ili baadae na sisi tuendeshe mambo yetu.
 
Watu wengine wa ajabu sana. Huku tunahimiza nchi za nje wake kuwekeza. Wakija (Kenya) mnasema tumepigwa. Mbona hamsemi hivyo kuhusu uwekezaji wa UK, South Africa au Mauritius? Magufuli aliharibu sana ajili za watu!
 
Watu wengine wa ajabu sana. Huku tunahimiza nchi za nje wake kuwekeza. Wakija (Kenya) mnasema tumepigwa. Mbona hamsemi hivyo kuhusu uwekezaji wa UK, South Africa au Mauritius? Magufuli aliharibu sana ajili za watu!
Wakenya mbwembwe tu hakuna kitu wanaishi maisha magumu kupita kiasi nusu ya ardhi yenye rutuba inamilikiwa na familia ya kenyata, hapo nairobi wanamiliki msitu mkubwa sana walipojenga kiwanda cha maziwa, hyo familia inamililki mahoteli, mabenki, kampuni za bima, shule, viwanda, mashamba, redio, tv stations, etc, uchumi wa kenya unamilikiwa na asilimia 0.5 ya wakenya wengi wao wakiwa ni wanasiasa, asilimia inayobaki ni mafukara wa kutupwa

Screenshot_20210427-224655.png


Screenshot_20210427-224708.png
 
Back
Top Bottom