Mkuu makampuni mengi ni ya uchochoroni, ambayo Yana fahamika hayazidi ata 50, anaweweseka na makampuni ya kulipa watu laki na nusu ahahahahahaha
Na nikwambie ukweli mtupu mkuu wangu 'ielewemitaa', shida inaanzia kwenye vikampuni hivyo vya mfukoni.
Hivi ni vikampuni vya wakubwa huko huko Kenya.
Hivi vikampuni vya mfukoni vinawapa shida wao kwelikweli, vinasumbua sana katika mambo ya rushwa wanaiita "tenderpreneur" huko kwao.
Vikampuni hivi ndivyo wanavyovitumia wakubwa walio serikalini na kwenye mashirika yao kufisadi hela ya serikali na misaada inayotolewa nchini humo.
Ukisikia 'scandal' zinazohusiana na uagizaji wa mahindi kwa mfano, kila mwaka nchi hiyo inapokumbwa na njaa, ni vikampuni hivyo ndio vinara wa kuvuruga taratibu zote za manunuzi ya kawaida. Ni hivyo hivyo na uagizaji wa sukari, kama ilivyokuwa mwaka juzi, hata tukapiga marufuku/tukaongeza ushuru kwa bidhaa zao zinazozalishwa kutokana na sukari, kama biskuti, icecream na pipi,n.k.; lakini wakalalamika kama watoto wadogo.
Juzi tu hapa, miezi michache iliyopita, wakapata misaada toka nje kupambana na COVID-19, wakubwa hawakuchelewa na vikampuni vyao, wakakwapua misaada hiyo kwa tenda magumashi zilizofanyika KEMSA (shirika lao la kununua na kusambaza vifaa vya tiba)
Ulishamsikia Gavana wao wa Kirinyaga, aliyewahi kuwa waziri wa vijana na ambaye sasa ni Gavana wa Kirinyaga Binti mzuri mzuri wa Kikuyu - Anne Waiguru. Yeye kasambaratisha mfuko wa kuwahudumia vijana akiwa waziri, na hakuna lolote lililofanyika.
Hii ni mifano michache tu ya hawa watu na vikampuni vyao wanavyovileta hapa.
Hatari iliyopo kwetu, wanaleta tabia zao hizi hapahapa, ndiyo maana sasa unawasikia akina Muhongo na wenzake huko Bungeni wakipiga kelele juu ya umeme wa gesi.
Tuwe waangalifu sana. Mambo haya yalishaanza kuota mizizi wakati wa Kikwete; inawezekana sasa wakaanzia walipoachia waliposambaratishwa na Marehemu Mgufuli.