Wakenya wametupiga bao sana kwenye uwekezaji nchini

Kuna msemo wa kiswahili, huwezi kutajirika kwa jirani yako. Tusiwe na matumaini makubwa sana. UCHUMI WETU UNAKUWA NA KARIBU TUTAWAKUTA ILA TUKIWAACHIA TANZANITE, UTALII, DHAHABU NA MADINI MENGINE WATAZIDI KUSONGA MBELE.

Mkuu,

Msemo huo ndiyo msingi wa umasikini wenyewe.
Ili uwe tajiri lazima ukachukue kwa jirani.
Bila majirani utajiri wako hauwezi kuongezeka (ref. Ukoloni na mendeleo ya nchi za magharibi).
Ukoloni mamboleo ni muendelezo.
 
Kenya fursa ziko kibao hasa za usafiri wa mabasi mazuri ya daladala na mikoani bado kule vi hiace ndio daladala na vi bus vya safari ndefu ya mkoa hadi mkoa mikoa mingi tu..
Tanzania Bus investors fursa hiyo mnajua ki hiace kilivyo kidogo fikiria upande hiace toka Dar hadi Arusha utafika miguu imeganda kawekezeni kenya.Njia vinaenda vi hiace ziko kibao nendeni nairobi tu pale mtapata information zote kwa nacho yenu Hamuhitaji kuajiri expert
 
Ongeza na Wakikuyu😃
 
Watz wangekuwa wanafikiria hivi,wangekuwa mbali sana,ata sisi wakenya tulijifunza kutoka kwa Wahindi na wasomali
 
Na hizo kampuni 30 si ajabu ukakuta 28 ni za watanzania wenye asili bara la asia.. sie tumekalia maneno tu hakuna tunachofanya productive

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Matatuu inajulikana worldwide
Imekuwa kivutio cha watalii

Bora sisi tungeacha chai maharage tu

Ova
 
sijakuelewa mkuu, sisi tuna kampuni 30 kenya au?
 
Matatuu inajulikana worldwide
Imekuwa kivutio cha watalii

Bora sisi tungeacha chai maharage tu

Ova
kivutio cha watalii malofa billy gate na mabilionea waweza panda chai maharage? na wanakuja mara moja moja tu mtu una suti utapanda chai maharage? kenya public transport bado haiko vizuri kabisa chama cha wamiliki wa daladala vamieni soko la kenya la ndani liko wazi mno nchi nzima.Vi hiace ndio eti usafiri wao
 
KENYA YUKO TU MBELE YA PAZIA UJUE KUWA NYUMA YA PAZIA HIZO ZOTE NI KAMPUNI ZA U.S.A NA U.K ZILIWEKEZA MITAJI KENYA WAKATI ZIKISUBILIA UJAMAA UANGUKE TANZANIA ULIPOANGUKA NDIO ZIKAVUKA MPAKA. FAIDA KWA WAKENYA NI KUWA ZILIWAPATIA UJUZI WA KUSIMAMIA MAKAMPUNI SASA BAADA YA KUJA TANZANIA HAZIONI SABABU YA KUIGIA TENA GHARAMA KUTOA UJUZI KWA WATANZANIA BALI WALETE WAKENYA WAKASIMAMIE KAMPUNI ZAO NA HAPA SERIKALI YA TANZANIA NDIPO INATAKIWA KUWA MACHO KWELI KWELI
 
Kenya ni Taifa kubwa la Uchumi Afrika Mashariki na Afrika.

Pili mnapokuwa na Rais dizaini ya Nyerere na Magufuli wanaotaka kufukarisha watu wao na kuwafanya tegemezi kwa serikali huwezi pata raia wabunifu,wathubutu na aggressive kwenye biashara .

Mwisho lugha ya biashara ni English ila hao wawili hapo juu wanashadidia kiswahili
 
Kama Taifa tufike mahala tuwe na sera za Uchumi na siasa ya uchumi inayoeleweka sio huyu anataka serikali ndio iwe kiongozi mwingine anataka private sector sasa hatuelewekagi tunataka nini hii nchi
 
Kwa nini mnang'ang'ania kiswahili na centralization kama unajua haya?
 
Kuna msemo wa kiswahili, huwezi kutajirika kwa jirani yako. Tusiwe na matumaini makubwa sana. UCHUMI WETU UNAKUWA NA KARIBU TUTAWAKUTA ILA TUKIWAACHIA TANZANITE, UTALII, DHAHABU NA MADINI MENGINE WATAZIDI KUSONGA MBELE.
Unachekesha mkuu,miaka 5 iliyopita gap Kati ya Kenya na Tzn imeongezeka hiyo kuwakuta watakuwa wanakusubiria wewe?
 
Unachekesha,kuanzia leo jua kwamba gap imeongezeka hizo ndoto za kuwakuta sahau,Ghana walikuwa nyuma yetu leo vipi?

Pili kusaport private sector unajua ni kufanyaje? Ni pamoja na kuondoa vikwazo vya biashara na kuwa na kodi rafiki.

Nchi hii haieleweki siasa yake kwenye swala la uchumi na tuna viongozi ambao hawawezi kusupoort biashara.mfano wakati kuna mzozo wa biashara Kati ya Kenya na Tzn ,,wanasiasa uchwara kila mtu alikuja na tamko na kujitutumua ikaishia kutupa hasara
 
kenya wamewekeza vitu vidogo dogo kama maduka ya madawa na bar nkTanzania kampuni chache lakini za nguvu
Wewe huwa ni empty fuvu ,kama ni tuvitu tudogo hiyo value ya biashara inazungumza nini? Gawanya kwa idadi afu utapata jibu
 
Tanzania ilikuwa ina Uchumi mkubwa kuliko Kenya, kabla ya USSR kuanguka.

Vita ya Kagera ndio iliangusha uchumi wetu, lakini kuanzia miaka ya 2000 uchumi wetu umekuwa sana, na hadi sasa wametupita kidogo sana.

Elimu ya Tanzania ni bora mara 100 ya Elimu ya Kenya, hili nina hakika nalo sana sana.

Shida ya Tanzania, ni Simba aliyelala, Watanzania ni watu wa sawa tu, hawataki kuipenda nchi yao ya kuipigania.

Kenya huwezi kukuta duka la mkikuyu linauzwa na Mjaluo au asiyemkikuyu, hadi bank watu wanahudumiana kilugha, hii ni moja ya sababu ya hayo maendelo ya Kenya.
 
Issue me naiona resource zipo kwetu nyingi ndio maana wapo wengi kwetu..utaenda kenya ukafanye nini..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…